Header Ads Widget

RC SERUKAMBA:ELIMU YA SHERIA NA UCHUMI MKOMBOZI KWA WANAWAKE NA VIJANA

 


Na Zuhura Zukheri Matukio Daima 

Mkuu wa mkoa wa Iringa Peter Serukamba amesema elimu ya sheria na uchumi itawakomboa wanawake na vijana katika kusianzisha na kusimamia biashara watakazokuwa wanazifanya katika maeneo yao.

 Serukamba aliyasema hayo leo  wakati akifungua kongamano la wanawake, vijana na Uchumi lilotandiliwa na BLS INITIATIVE nakuudhuriwa na zaidi ya vijana na wanawake 200 kutoka maeneo mbalimbali mjini Iringa wakiwemo wanavyuo.


 Serukamba alisema kuwa wanawake na vijana ni uti wa mgongo wa maendeleo hivyo wakipata elimu ya uchumi maarifa na sheria  huwa ni chachu ya maendeleo chanya katika familia, jamii na taifa kwa ujla kwa kuwa lina endana lengo la serikali la kuwezesha kila mwananchi kushiriki maendeleo kwa taifa.

Alisema kuwa kuna umuhimu wakuwajengea uwezo wa kiuchumi na kisheria kwani wanawake wanatakiwa kujua haki zao za kiuchumi na kisheria kwakuwa teknolojia ya sasa inataka watu hasa wanawake na vijana kuwa na uwezo wa kujitegemea kiuchumi.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanawake na vijana wanapewa fusra za kiuchumi na kisheria ili kukabiliana na  changamoto za kimaisha    

Alisema kuwa jukumu la viongozi na watu binafsi ni kuhakikisha taarifa za uwezeshwaji wa kiuchumi na kisheria unawafikia watu mbalimbali hususani vijana na wanawake


“Kwa mukhtadha wa dunia ya sasa maarifa ya kiuchumi na kisheria ni silaha muhimu ya kupambana na changamoto ya maisha yetu ya kila sikuwanawake wanatakiwa kujua haki zao za kiuchumi ikiwemo haki ya kumiliki Ardhi kufanya biashara, na kupata mikopo ya riba nafuu.”alisema Serukamba

Aidha alisema vijana wanapaswa kuelewa mchakato wa kuanzisha na kuendesha biashara na kufahamu sheria wanapojihusisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Alisema jukumu la viongozi na taasisi binafsi kuona taarifa muhimu zinafika kwa wanawake na vijana kama walivyofanya BLS INITIATIVE 

“Ilikufanikisha malengo ya kuwawezesha wanawake na vijana ni lazima sekta ya umma na binafsi kushirikiana kwa karibu taasisi kama BLS INITIATIVE zinajukumu kubwa lakutoa elimu   mafunzo kushirikiana na serikali katika kuweka mfumo rafiki kwa maendeleo ya wananchi hususani wanawake na vijana na serikali yenu ya mkoa wa Iringa itashirikiana na BLS INITIATIVE katika juhudi za kuboersha maisha ya vijana na wanawake.”alisema Serukamba 


Akizungumza mwenyekiti wa bodi ya BLS INITIATIVE wakili Barbanas Nyalusi  alisema kuwa lengo la kuandaa kongamano hilo ni baada ya kuona wanawake na vijana wengi wamekuwa wakitamani kuanzisha biashara lakini hawana mitaji wala elimu ya uchumi na sheria.

Alisema kuwa watu wengi wanaishi katika jamii lakini hawazioni fursa zilizowazunguka na ndiomaana wametoa elimu hiyo ili wajue jinsi ya kuzitumia fursa zilizopo katika maeneo yao.

Alisema kuwa kutokana na changamoto za vijana na wanawake katika uendeshaji wa biashara ndio iliwasukuma kuitisha kongamano la kuwawezesha kufahanu haki zao.

“Ni seme na vijana msiogope kuwa juu ya waliofanikiwa kwa ni hata wao walianza wakiwa na mitaji midogo baadae wakakua hivyo wafuateni na muwaulize njia walizopitia wakafanikiwa niwambie tu tafuteni hela vitu vingine vyote vitakuja” alisema wakili Nyalusi.

Nyalusi alisema kuwa muitikio wa walengwa wa kongamano ulikuwa ni mkubwa kuliko walivyotarajia huku idadi kubwa ikiwa ni vijana kutoka katika jamii na vyuoni.


 Nao wawasilishaji wa mada wamewataka washiriki wa kongamano hilo kuanza kuwa na wivu wa kimaendeleo kwa kuchangamkia fursa, kutunza fedha Pamoja na kuweka akiba yenye malengo ya kimaendeleo huku.

Wamesemakuwa katika maisha mtu anatakiwa kuwa na tabia ya kuweka akiba ambayo inamalengo na sio kuweka akiba bila malengo ambayo utaitumia katika vitu visivyo na umuhimu.

Dr. Anne wakati akiwasilisha mada ya sheria aliwataka wanawake kuanza kujifunza masuala ya sheria hasa katika sheria ya umiliki wa ardhi ambayo wanawake wengi wamekuwa wahanga wa kudhulumiwa ardhi hasa pale mwenza anapofariki au kutalikiana.

Alisema kuwa umiliki na uuzaji wa ardhi uanasheria zake ambazo mwanamke anahusika katika maamuzi ya uuzaji wa ardhi jambo hilo wanaume wengi wamekuwa hawaliafiki.

“Wanawake wamekuwa ni wahanga wa kudhulumiwa pindi mwanaume anapotaka kuiuza kwani sheria inamtaka kuwa napicha ya kwake na ya mkewe katika mkataba wa mauziano lakini wanaume wengi kwa kulikwepa hilo wanaenda kutafuta picha ya mtu baki nidio wanaweka huu ni udhulumaji.”alisema dr. Anne

Nae msemaji  wa wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga taifa Zeche Zebron aliwataka vijana na wanawake kuwa na uthubutu wa kuanza biashara kwa mtaji mdogo huku akiwatahadharisha kuchukua mikopo bila malengo ikiwemo mikopo ya kausha damu.

Alisema kuwa mtu akiwa na mtaji wa shilingi 30,000 anaweza kuanzisha biashara ndogondogo na mtaji ukakua kila siku inategemea na ubunifu wa mfanyabiashara.

Aidha alisema kuwa wafanyabiashara wengi wamekuwa wakishuka kibiashara kutokana na kushindwa kuwa na lugha ya kibiashara pindi anapofika mteja na kukwama kununua.


“ mimi wakati na naanza biashara nilikuwa na mtaji wa elfu 30000 nikachukua nguo nikaanza kutembeza vyuoni biashara ile ilikuwa nikafungua banda wenzangu walikuwa wakija wateja wakijaribisha nguo wasiponunua wanakasirika lakini mimi nilikuwa nawachangamkia nawatolea na nguo zingine basi nikawa na pata wateja leo hii nimekuwa na ninaduka la kukopesha hela.”alisema Zebron

Nao washiriki wakongamano wamewashukuru waandaaji wa kongamano hilo BLS nakuomba wadau wengine kujitokeza kudhamini na kuandaa makongano kama hayo ambayo yanaenda kufungua akili za vijana wengi hasa wanachuo wanao waza kuajiriwa badala ya kujiajiri.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI