Header Ads Widget

RC MALIMA ALIVYOPIGA KURA

 


MKUU wa Mkoa wa Morogoro Bw Adam Malima amesema tayari ametoa maelekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo mbalimbali hasa ya wilaya za Kilombero, Kilosa na Mvomero kushughulikia changamoto ya uchelewaji wa vifaa kwa uchaguzi kwa baadhi ya maeneo hali iliyosababisha uchaguzi kushindwa kufanyika kwa wakati.


Mkuu huyo wa Mkoa alisema hayo baada ya kutimiza haki yake ya Msingi na ya Kikatiba ya kupiga kura katika kituo cha LITI manispaa ya Morogoro.


Baadhi ya maeneo ya wilaya hizo ikiwemo Dumila mjini na Kidatu, uchaguzi uliripotiwa kuchelewa kuanza kutokana na kuchelewa kuwasili kwa vifaa.


Aidha baadhi ya maeneo ya mjini Morogoro baadhi ya wananchi akiwemo Bw Juma Hassan mkazi wa mtaa wa Mgaza, kata ya Mindu walishauri Serikali iwe inatoa elimu ya  Uraia itakayoainisha pia umuhimu WA watu kujitokeza kupiga kura ili kuchagua viongozi wao tofauti na sasa mwamko wa wananchi umekuwa ni mdogo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI