Na,Jusline Marco :Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amesema uchaguzi wa serikali za mitaa ndiyo sehemu pekee inayompa uhuru na mamlaka mwananchi mwenye sifa katika kuchagua kiongozi na kuunda serikali aitakayo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura katika kituo alichojiandikishia vha AICC Hospital Mtaa wa Mahakamani Kata ya Sekei Jijini Arusha , Makonda zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa ni zoezi muhimu katika nchi linalompa kilq mwananchi uhuru wa kushiriki kuunda serikali anayoitaka.
Aidha ameongeza kuwa suala la kulinda kura baada ya kupiga kura linabaki kwa mawakala kulingana na kila chama cha siasa kilivyoweka mawakala wake ili matokeo yatakapo kamilika wakala ndiye shahidi wa kwanza.
Sambamba na hayo Mkuu huyo wa Mkoa amesema hivi karibuni Mkoa wa Arusha utapokea ugeni wa marais zaidi ya wanane huku mwenyeji wao akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan hivyo amewataka wananchi kuendelea kuilinda amani ya Mkoa wa Arusha na kutumia fursa hiyo kwa kufanya biashara na kujiingizia kipato.
Jiji la Arusha lina jumla ya vituo vya kupigia kura 462 huku Waliojiandikisha kupiga kura wanaume wakiwa 176,150 na Wanawake 173,561 Sawa na asilimia 88.3.
0 Comments