Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Kenan Kihongosi amemuagiza katibu Tawala Mkoa wa Simiyu kumhamisha mara moja kituo cha Kazi Afisa Kilimo wa Wilaya ya Meatu Bw. Thomas Shilabu kwa kushindwa kutekeleza majukuku yake kikamilifu.
Aidha Mhe.Kihongosi amemuagiza katibu Tawala Mkoani Simiyu kuwabadilishia vituo vya kazi wakuu wa Idara na Sehemu wote ambao wamekaa muda mrefu katika vituo vyao vya kazi ili kuimarisha utendaji kazi ndani ya Mkoa wa Simiyu.
Hatua hiyo inajiri baada ya baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mwabusalu kutokuwa na taarifa kuhusu uwepo wa ruzuku katika mbegu za mahindi wakiiomba serikali kuwapatia mbegu hizo kwa ruzuku.
Mhe.Kihongosi yuko katika ziara ya siku 2Wilayani Meatu kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za Wananchi.
0 Comments