Header Ads Widget

NCAA KUJIPANGA KUIMARISHA VIVUTIO VYA MALIKALE NCHINI

Na,Jusline Marco,Tanga.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imejipanga kuhakikisha inalinda, inahifadhi na kuimarisha vivutio vya malikale inavyovisimamia.

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka hiyo Dkt.Elirehema Doriye ameyasema hayo wakati akizungumza mara baada ya kutembelea Mapango ya Amboni Mkoani Tanga yanayosimamiwa na Mamlaka hiyo.

Dkt.Doriye amesema mapango ya Amboni ni moja ya vituo vya malikale ambayo Mamlaka hiyo imedhamiria kuhifadhi, kuendeleza, kuboresha na kuyatangaza zaidi ili kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea mapango hayo.

Ameongeza kuwa kwa sasa NCAA inaendelea kupanua wigo wa mazao mapya ya utalii ili kuongeza vyanzo vya mapato na kuongeza mtawanyiko wa wageni hasa katika vituo vya malikale.

Mapango ya Amboni ni moja ya vituo vya malikale vinavyosimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambayo yamebeba historia kubwa ya harakati za kudai uhuru Nchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI