Header Ads Widget

MRADI WA MAKUMBUSHO YA JIOLOJIA YA NGORONGORO-LENGAI KUNUFAISHA WATALII NA WAKAZI WA MAENEO YANAYOZUNGUKA MRAFI HUO.

Na;Jusline Marco;Arusha

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt.Pindi Chana amesema Serikali kupitia wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kuhakikisha inafikisha idadi ya watalii milioni 5 watakaotembelea vivutio vya utalii katika hifadhi za taifa nchini.

Balozi Dkt.Chana ameyadema hayo wakati akiweka jiwe la Msingi la Mradi wa Makumbusho ya Jiolojia ya Ngorongoro-Lengai unaofadhiliwa na Serikali ya Watu wa China ambapo amesema  hadi sasa tayari watalii wasipungua elfu 54 kutoka nchini mbalimbali ikiwemo China wametembelea hifadhi za taifa nchini.

Aidha amesema kupitia uongozi bora wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan mataifa mbalimbali yamekuwa yakishirikiana na Tanzania katika uwekezaji kwenye sekta mbalimbali na amekuwa akiacha alama katika kila sekta ikiwemo Elimu,Afya na Utalii pamoja na sekta nyingine.

Ameongeza kuwa jengo hilo la Makumbosho  linaakisi mila na desturi za jamii ya wamaasai na bonde la Hifadhi ya Ngorongoro huku maeneo ya utalii wa miamba na jiolojia yakihusisha milima,maziwa na mandhari mengine ya asili ambayo Tanzania imeendelea kuyalinda na kuyatumia ipasavyo.

Kwa upande wake Meneja wa Idara ya Urithi wa Utamaduni wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Msimamizi wa Mradi wa Hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro Lengai Dkt.Agnes Gidna amesema mradi huo unaohusha uendelezaji wa maeneo ya Jiolojia yanayopatikana ndani ya hifadhi ya Ngorongoro na kukuza utalii wa miamba.

Dkt.Agnes amesema mradi huo una awamu mbili za utekelezaji ambazo zitatumia kiasi cha shilingi Bilioni 22 hadi kukamilika kwake ambapo awamu inahusu ufanyaji utafiti wa maeneo yote yaliyo ndani ya hifadhi ambao ulianza Juni 2023 na kutarajiwa kukamilika Oktoba 2025 huku awamu ya pili ikihusisha Ujenzi ambao unaendelea kwa sasa.

Naye mwakilishi wa Katibu Mkuu,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Felista Lugambwa amesema mradi huo unatokana na mahusiano mazuri baina ya China na Tanzania na nisehemu ya miradi ya Focac ya 9 ambayo Tanzania ni miongoni mwa nchi iliyoshiriki vikao mbalimbali kupitia jukwaa la Jukwaa la Ushitikiano Focac. 

Kwa upande wake Balozi wa China Nchini Tanzania Mhe.Chen Mingjian kama watekelazi wa mradi huo wameahidi kukamilisha mradi huo kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa kwani utekelezaji wa mradi huo unatokana na uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya China na Tanzania.

Sambamba na hayo Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Elirehema Doriye amesema Mradi huo wa miamba utakapokamilia utasaidia watalii Kutoka mataifa mbalimbali kufurahia kutokana na vivutio Vitakavyokuwemo katika makumbusho hayo huku wakazi wa maeneo hayo wakiwa sehemu ya  wanufaika wa mradi huo.

Awali akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mtendaji wa Unesco Tanzania Prof.Hamis Malebo amesema Unesco imeendelea kuisaidia hifadhi ya miamba ya Lengai ambayo mpaka sasa hivi wameweza kuboresha mambo mengi ambayo yataipelekea kuwa hifadhi ya kipekee katika Afrika na Dunia kwa ujumla.






 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI