Header Ads Widget

MNEC SALIM ASAS AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA KUCHAGUA VIONGOZI BORA


Na Matukio Daima media 

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Asas, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kesho kushiriki kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji, na Vijiji ili kuhakikisha maendeleo yanaendelea kusimamiwa ipasavyo.


MNEC  Asas amesema kuwa ni muhimu kuchagua viongozi bora ambao watatekeleza kwa ufanisi dira na mipango ya maendeleo inayosimamiwa na serikali iliyopo madarakani chini ya Chama Cha Mapinduzi. 

Kuwa CCM imekuwa mstari wa mbele katika kupambania maendeleo kwa wananchi wa Tanzania kwa kuanzisha na kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati inayogusa maisha ya kila mwananchi.


“Asilimia kubwa ya miradi mikubwa ya maendeleo nchini, ikiwemo ujenzi wa barabara, shule, hospitali, na maboresho ya miundombinu ya maji na umeme, imetekelezwa na serikali ya CCM Ili miradi hii iwe na tija sasa na kwa vizazi vijavyo, ni lazima isimamiwe na viongozi bora kutoka CCM hii ndio sababu wananchi hawapaswi kupuuza uchaguzi huu,” alisema Asas.

Pia alitoa wito kwa vijana kushiriki kwa wingi, akisisitiza kuwa wao ndio msingi wa mabadiliko katika jamii. 

Alisema kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatoa nafasi ya kipekee ya kuhakikisha viongozi wenye maadili mema, uadilifu, na uwezo wa kusimamia rasilimali za umma wanachaguliwa.

“Kesho ni siku muhimu kwa maendeleo yetu hakikisha unapiga kura yako kwa viongozi wanaostahili, hasa wale wanaotokana na CCM, chama chenye historia ya kusimamia maendeleo ya kweli,” alihitimisha.

Wananchi wameendelea kuhamasishwa kushiriki uchaguzi huu ili kuimarisha demokrasia na kuhakikisha maendeleo yanadumu katika ngazi ya jamii.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI