Na Matukio Daima media
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji, na Vijiji ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi yetu.
Jasmine Ng’umbi ni mjumbe Kamati ya Utekelezaji UVCCM Wilaya ya Mufindi
Anasema kuwa uchaguzi huu ni fursa kwa wananchi, hususan vijana, kushiriki katika maamuzi ya msingi yanayogusa maisha yao moja kwa moja.
Kupiga kura katika uchaguzi huu ni hatua ya uwajibikaji na njia madhubuti ya kuleta mabadiliko chanya.
Anasema kwanza, kupiga kura kunawapa wananchi uwezo wa kuchagua viongozi bora wenye dira na uwezo wa kusimamia maendeleo ya jamii.
Viongozi wa mitaa na vijiji wana nafasi ya moja kwa moja katika kuboresha huduma za kijamii kama elimu, afya, maji safi, na miundombinu.
Ng'umbi anasema kupiga kura kwa umakini kunahakikisha watu waadilifu wanapewa nafasi ya kuleta mabadiliko.
Pili, ni njia ya kukuza demokrasia na uwazi katika jamii.
Kwa kushiriki uchaguzi, vijana na watu wote wenye sifa wanatoa ujumbe kwamba wanathamini haki yao ya kidemokrasia
"Kwa hii huchochea uwajibikaji wa viongozi waliochaguliwa kwa sababu wanajua wanalazimika kuwajibika kwa wapiga kura waliowapa nafasi"
Tatu, vijana wanaposhiriki uchaguzi wanajiwekea msingi wa kuwa sehemu ya maamuzi yanayoathiri maisha yao na kizazi kijacho.
Anasema kuwa hii huwapa sauti na nafasi ya kuleta mawazo mapya yenye lengo la kuboresha maisha ya jamii kwa ujumla.
Ikumbukwe kupiga kura ni wajibu wa kikatiba ambao unawaunganisha wananchi wote katika kutekeleza ndoto ya taifa lenye mshikamano na maendeleo.
Kwa kutumia haki hii, tunalinda uhuru wetu wa kisiasa na kuhakikisha nchi yetu inatawaliwa kwa njia ya haki.
Jasmine Ng'umbi anasema wananchi wote wenye sifa, msikubali kupoteza haki hii muhimu iwapo ukijiandikisha kwenye daftari la mkazi p, shiriki, na hakikisha unapiga kura ili kuleta maendeleo yanayoendana na matarajio yako na jamii kwa ujumla.
"Niwaombe sana twendeni kupiga kura kwa wingi tuchaguzi viongozi makini na Bora kutoka CCM kwani ilani ya Uchaguzi ya CCM itasimamiwa vizuri na viongozi toka CCM na Chama kina nafasi ya kuwabana tofauti na kuweka kiongozi nje ya CCM ambae ni vigumu kumwajibisha "
Kuwa miradi inayotekelezwa na serikali yetu chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni miradi iliyotajwa kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM na mwenye kusimamia miradi hiyo ni lazima atokane na Chama chenye ilani yake .
Hivyo niwaombe watanzania wote tusifanye Makosa katika kuchagua viongozi lazima kutambua unamchagua akakufanyie nini kama ni maendeleo Soma hitaji la ilani ya Chama chake ni ilani ya Kuleta maendeleo kabla ya kuchagua vinginevyo usiumize Kichwa ilani ya CCM imenyoka sana na tayari Matunda yanaonekana piga kura yako Kwa viongozi wa Chama Cha mapinduzi.
0 Comments