Header Ads Widget

MJASIRIAMALI HUSSEIN MDARI AWALILIA VIONGOZI WA MKOA WA TANGA KWA MSAADA WA MTAJI


 Na Matukio Daima App 

Mjasiriamali Hussein Mdari kutoka Mkoa wa Tanga, anaiomba serikali na viongozi wa mkoa huo kumsaidia kwa mtaji wa biashara, baada ya kukumbwa na hali ngumu ya kifedha. Hussein anasema alikopa fedha milioni kumi kutoka benki kwa ajili ya kuendeleza biashara zake, lakini alikumbwa na janga la kuibiwa kiasi hicho cha fedha pamoja na mtaji wake, hali iliyopelekea kushindwa kusimamia biashara hiyo.

Akizungumza na mwandishi wetu, Hussein anasema: “Naomba msaada kutoka kwa serikali yangu ya Mkoa wa Tanga, pamoja na viongozi wangu wa chama cha siasa, hususan Mwenyekiti wa Mkoa, Mheshimiwa Abdallahman Rajab. Hii ni ili niweze kuinuka tena na kuendelea na shughuli zangu za kimaisha, hasa kuwahudumia watoto wangu ambao mke wangu aliniachia baada ya kutoroka na fedha milioni kumi."

Hussein ameongeza kuwa, "Ninaamini kupitia serikali yangu inayoongozwa na Mkuu wa mkoa wetu hapa Tanga Mama Barozi Batilda Burihani, na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Ndugu Japhari Kubecha, wanaweza kunisaidia kwa namna moja au nyingine ili niweze kujikwamua na kurejesha hali yangu ya kifedha."

Mjasiriamali huyo amesema, kwa sasa benki inamdai na wanataka kuuza nyumba aliyojenga kwa ajili ya familia yake ili kufidia deni. "Hali yangu ni mbaya, lakini bado naimani kuwa msaada utapatikana. Hata Mheshimiwa Hummy Mwalimu aliguswa na shida yangu na kunilipa kodi ya fremu ya biashara. Namshukuru sana kwa msaada wake," alisema Hussein.

Pia, alitumia fursa hii kuomba msaada kutoka kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, akisema: "Nikiwa kada wa chama cha Mapinduzi, naomba msaada wa dhati kutoka kwa viongozi wangu ili niweze kusimama tena na kumudu maisha yangu."

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI