Header Ads Widget

ASKARI WA UHIFADHI MKAWAJIBIKE IPASAVYO, MUIPELEKE TANAPA VIWANGO VYA JUU - KAMISHNA MWISHAWA

 



Na. Brigitha Kimario- Serengeti 


Askari Uhifadhi 124 wapongezwa na kuhimizwa kuzingatia waliyofundishwa katika kipindi chote cha mafunzo, kuyafanyia kazi kwa bidii, lengo kubwa likiwa ni kuipeleka TANAPA katika viwango vya juu kiuhifadhi na kiuchumi “Tanapa next level”.


Hayo yamesemwa na Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara, Massana Mwishawa leo tarehe 11.11.2024 wakati akihitimisha mafunzo ya Awali ya ajira mpya katika Kituo cha Mafunzo kinachomilikiwa na Pasiansi, Fort Ikoma Serengeti.


Kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi TANAPA Naibu Kamishna Mwishawa alisema nina imani kuwa mafunzo haya yamewajengea uzalendo, uadilifu, ujasiri, utayari, kujiamini pamoja na kuwapa mbinu na ari kubwa katika kulinda Maliasili za Taifa. Hivyo, mafunzo mliyoyapata yasiishie hapa bali mkayaishi kwa vitendo wakati mkitekeleza majukumu yenu ya kila siku kwenye vituo vyenu vya kazi.

 

"Niwaase wote muepuke kujihusisha na vitendo visivyofaa kwenye uhifadhi ikiwemo vitendo vya rushwa na matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima wakati wa kutekeleza majukumu yenu ya kila siku".


Aliongeza kusema nina imani kupitia mafunzo haya mtakuwa mmejengewa uwezo wa kusimamia rasilimali hizi za wanyamapori na misitu ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa. 


Naye, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Betrita Lyimo ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Kaskazini alisema nimefurahishwa sana na ukakamavu mlionao, tumejionea kweli mmeiva . Mkalitumikie jeshi la uhifadhi kwa ujasiri, ukakamavu huu huu mliooonyesha, msibweteke mkifika kwenye vituo vyenu vya kazi.


“Mliyoonyesha leo muendelee nayo mkajitume, mkawajibike ipasavyo huku mkifuata sheria, kanuni na taratibu za kazi. Na Mungu atawasaidia”. Alisema Kamishna Betrita 


Aidha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Izumbe Msindai ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Magharibi alisema nitumie nafasi hii kuwaasa kujenga umoja na ushirikiano baina yenu askari na maafisa, ushirikiano huondoa migawanyiko katika kazi. 


“Ushirikiano ni mzuri, tunakushukuru Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi Bw. Jeremiah Msigwa kwa kutoa nafasi ya mafunzo kufanyika katika chuo hiki pamoja na kuruhusu wakufunzi wako kushirikiana nasi bega kwa bega kufundisha baadhi ya masomo kwa wahitimu hawa.


“Tumefurahi leo wahitimu wamekuwa wakakamavu na mahiri, mazoezi ya utimamu yameonesha kuwa mmeongeza ujuzi na mtakuwa weledi katika kazi".


Mafunzo haya yaliyohitimishwa ni mafunzo ya awali ya ajira mpya (WFCS Recruit Course) kwa Askari wa Uhifadhi 124 intake ya 10 wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania -TANAPA.







00


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI