Header Ads Widget

MBUBGE SICHALWE AHIMIZA WANANCHI KUJITOKEZA KUSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

 

Na Thobias Mwanakatwe, Momba 

MBUNGE wa Jimbo la Momba mkoani Songwe, Condester Michael Sichalwe  amewataka wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba kujitokeza kwa wingi kushiriki kampeni na uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27, 2024.


Alisema hayo  16 Novemba 2024 akiwa katika  kata ya Ivuna wakati akizumgumza na mamia ya wananchi walijitokeza katika mashindano ya Condester Cup 2024 ambayo yanafanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Ivuna .

Sichalwe alisema uchaguzi wa Serikali za Mitaa   ni muhimu sana katika kuwapata viongozi wazuri hasa ambao tayari wamepitishwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili waweze kuwachagua kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya wilaya hiyo,mkoa na taifa kwa ujumla.

"Niwaombe sana vijana wenzangu tuliopo hapa  tukawe mstari wa mbele kwenda kupiga kura, maana kwa kufanya hivyo tutapata viongozi wazuri watakaotuvusha kwa kipindi chote cha miaka mitano.


Alisema wakati kampeni zinakwenda kuzinduliwa hivi karibuni tujitokeze pia kusililiza sera nzuri za wagombea wetu, tusiwaachie wazee tu kwenda kupiga kura na sisi vijana ni jukumu letu na haki yetu kuchagua na kuchaguliwa.

Aidha, mbunge Sichalwe alizngumzia mafanikio ya miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo yamefanyika ndani ya jimbo la Momba na kumshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi za maendeleo ambazo zimeletwa katika jimbo hilo.


"Jamani wana Momba tuseme ukweli, kila mtu nishahindi hapa, Momba ya leo siyo kama ya jana, ndani ya kipindi changu cha miaka mi Nne ya Ubunge wangu tumekuwa na mabadiliko makubwa ndani ya jimbo letu, barabara zinapitika, huduma za afya zimeborshwa kwa kiasi kikubwa, miundombunu ya elimu inavutia, umeme unaendela kusambaa mpaka vitongojini," alisema Sichalwe.


Baadhi ya wananchi, hasa vijana ambao ni wapenda soka wamemshukuru Mbunge wawo kwa kuwa mhasisi wa mashindano hayo ya Condester Cup msimu wa tatu, kwa madai kuwa yamewasaida kufahamiana vizuri na kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi miongoni mwao.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI