Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Timu sita za kata ya Madilu wilaya ya Ludewa mkoani Njombe zimeanza kutimua vumbi katika mashindano yaliyozinduliwa leo chini ya udhamini wa kampuni ya Jolam Property.
Timu shiriki katika ligi hiyo ni pamoja na Manga Fc,Mfalasi Fc,Matundu Fc,Madilu Fc,Ilininda Fc na Ilawa Fc
Akizindua Mashindano ya kata hiyo mgeni wa Heshima Josaya Luoga ambaye ni katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe na mkurugenzi wa Kampuni hiyo amesema kampuni hiyo iliamua kudhamini ligi hiyo ili vijana wapate nafasi ya kujiweka timamu kimwili na kiakili kupitia mashindano hayo yatakayotamatika kwa kutolewa zawadi mbalimbali.
Kwa upande wake mkurugenzi mwenza wa kampuni ya Jolam Property inayojihusisha na masuala ya ardhi bwana Lawi Mnyanga amesema michezo hiyo itawasaidia vijana kujiepusha na vitendo viovu ukiwemo ulevi na ngono zembe kwa kuwa muda mwingi watautumia kucheza michezo.Naye Diwani wa kata ya Luana Wilayani Ludewa Wilbard Mwinuka ameiomba kampuni hiyo kuendelea kufadhili katika nyanya nyingine pia zikiwemo za Afya na Elimu.
Sanjari na michezo hiyo lakini pia Ligi hiyo inahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
0 Comments