Na Esther Machangu, Moshi
Jamii imetakiwa kutambua na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili vijana wa kike katika kushiriki katika shughuli za Ufagaji hasa wa kuku Mkoani Kilimanjaro .
Hayo yameelezwa na washiriki wa semina za kuhamasisha wasichana kufanya ufugaji wa kuku akiwemo Reina Mrema katika semina hizo ambazo zinazoendeshwa na Maafisa mifugo wilaya (Hai & Siha) Kwa kushirikiana na watendaji wa kata, vijiji, maafisa kilimo na ufugaji, viongozi wa kimila na viongozi wa kidini kwa kushirikiana na taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mifugo (ILRI) na taasisi ya vijana ya Shujaaz.
Katika semina hizo zinazowalenga wasichana na pia zimewashirikisha na vijana wa kiume lengo likiwa ni kuangalia ni jinsi gani itakavyo ongeza chachu kwa vijana hao kushirikiana katika kutumiza lengo hilo.
Conjesta Pastory ni Afisa mifugo kitengo cha Mkuku wilayani Siha Mkoni kilimanjaro amesema mafunzo ya ufugani wa kuku yanatolewa na wadau yanasaidia sana kuwapa mbinu mpya wasichana wanaoanza kuingia katika ufugani huo hii ikiwa ni kwa namna ya kutambua mbinu mpya na kuongeza mnyororo wa thamani katika ufugaji wa Kuku kisasa.
Karingo saidi mvungi ni mwenyekiti wa Kijiji cha Ngarenairobi Wilayani Siha ameiomba serikali ya Awamu ya sita kuongeza juhudi katika kutoa mikopo kwa vijana ili waweze kushiriki kwa mapana shughuli hizo za ufugaji.
Naye Allan Lucky Komba kutoka Tasisi isiyo ya kiserikali ya SHUJAAZ amesema kwa kipindi ambacho wamefanya semina hizo wamegundua kuwa Mkoa wa Kilimanjaro una wanawake wanaopenda kujishughulisha katika sekta mbalimbali hivyo wakipewa nafasi wanao uwezo wa kufanya mambo makubwa katika jamii zao
Hata hivyo komba amesema Lengo kuu ni kubainisha changamoto zinazowakumba wanawake katika kilimo na ufugaji, kwa pamoja kama jamii, na kutafuta suluhu za changamoto hizo.
Mpaka sasa semina 8 zimefanyika katika wilaya ya Hai na Siha. Maeneo yaliyofanyika semina hizi ni pamoja na: Mtaa wa Amani, Mtaa wa Nyerere, Mtaa wa Uzunguni,Mtaa wa kibaoni, kijiji cha Kyeri, na kijiji cha Foo katika wilaya ya Hai, kijiji cha Lawate na kijiji cha Ngarenairobi katika Wilaya ya Siha. Semina nyingine mbili zitafanyika kwenye vijiji vya Merali na Karansi katika Wilaya ya Siha, kuhitimisha idadi ya semina 10 kwa Wilaya hizi mbili.
Baada ya mkoa wa Kilimanjaro, semina zitahamia Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
0 Comments