Na Fatma Ally Matukio DaimaApp, Dar
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imeitaka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Nov 27, mwaka huu unasimamiwa kwa haki na usawa ili kuondoa changamoto zinazoathiri michakato wa uchaguzi kila wakati nchi inapoingia katika chaguzi.
Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya CCT Askofu Dkt Fredrick Shoo wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukaa kikao cha kamati tendaji ya Jumuiya hiyo kilichofanyika ofisini kwao ambapo pamoja na mambo mengine kimejadili kwa kina hali ya kisiasa nchini.
Amesema kuwa, kumekua na malalamiko juu ya uandikishaji wa wawapiga kura wasiokuwa na sifa, kutofuatwa utaratibu na muda mfupi wa uandikishaji wa siku saba tu hali iliyopelekeanchi watu walio nasifa kushindwa kupiga kujiandikisha, pia baadhi ya watu kuonekana kutokidhi vigezo Kwa mujibu wa sheria, mfano majina ya watu waliofariki bado yapo kwenye daftari na wengine kutoka na umri stahiki.
"Kuenguliwa kwa wagombea kwa sababu ndogo za kiufundi, vikwazo katika kuchukua na kurejesha fomu za wagombea, mapingamizi ya rufaa, kutekwa, kujeruhiwa , kupotea na kuuwa kwa wananchi kunakohusiana na masuala ya siasa na uchaguzi yote haya ni changamoto zilizobainika katika maandalizi ya Uchaguzi "amesema Askofu Dkt Shoo.
Hata hivyo, amevitaka vyama vya siasa kufuatilia na kusimamia kampeni za wagombea kutoka katika vyama vyao na kuhimiza ustarabu na kuelimisha katika kunadi sera za chama husika bila kutumia lugha mbaya za matusi/Maudhi zinazoweza kuhatarisha amani ya nchi.
"Tunahamasisha vyama vyote vinavyowania nafasi za uchaguzi kuweka mawakala waadilifu katika kusimamia zoezi zima la upigaji wa kura, kuhesabu, kujumlisha na kutangaza matokeo ili kuepuka sintofahamu baada ya Uchaguzi na kutupiana lawama"amesemaAskofu Dkt Shoo.
Aidha, amesema kuwa mgombea ambae hana mpinzani sheria inaelekeza apigiwe kura ya NDIYO na HAPANA ili kutoa haki kwa wananchi kuchagua viongozi wanaowataka na sio kupitishwa bila kupingwa, huku akiwataka waumini wote kumtanguliza Mungu mbele katika kipindi hiki muhimu wanapoelekea katika uchaguzi kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Taifa.
Sambamba na hayo amewaka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wa kijamii wa mtaa, Kijiji na kitongoji wenye sifa sio kwa ushabiki wowote ule , huku akiwataka waendelee kudumisha amani na mshikamano wakati na baada ya Uchaguzi.






0 Comments