Header Ads Widget

WHI YATUNUKIWA TUZO YA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU AFRIKA

 


Na Fatma Ally Matukio DaimaApp

Watumishi Housing Investment (WHI) imetunukiwa tuzo ya Nyumba za Gharama Nafuu zaidi Afrika iliyotolewa na Taasisi ya Mikopo ya Nyumba Afrika (Afrika Union for Housing Finance AUHF) inayotambuliwa  na Umoja wa Afrika (Africa Union)ambapo tuzo hiyo imetolewa katika mkutano mkuu wa AUHF mwaka 2024 uliofanyika Zanzibar hivi Karibuni.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa WHI  Dr Fred Msemwa amesema kuwa tuzo hiyo ya heshima inatambua jukumu la WHI katika kuiwezesha umiliki wa nyumba kwa watu wa kipato cha chini na kati nchini Tanzania na juhudi zilizofwnywa na WHI katika kuleta suluhisho la njia nafuu za malipo za nyumba.


"WHI katika kuleta suluhisho la njia nafuu za malipo za nyumba ikiwemo malipo endelevu yanayolipwa kipindi cha ujenzi bila riba pamoja na utaratibu wa mpangaji, mnunuzi ambavyo vilitajwa kama sababu kuu za ushindi huu njia hizo zimeleta unafuu mkubwa sana kwa watu wanaotamani kumiliki nyumba"


Amesema kuwa,nyumba za WHI zinauzwa kwa bei nafuu kwa kati ya asilimia 10 hadi 30 ukilingalishwa na nyumba kama hizo kwenye soko, huku bei ya kununua nyumba ikianzia shill mill 38, bei hizo pamoja na njia nafuu za malipo zimewasaidia watanzania wengi kufikia ndoto zao za kumiliki nyumba.


Ameongeza kuwa,Taasisi hiyo imekua ya kwanza nchini na Afrika Mashariki kupokea tuzo hiyo ya heshima, huku ikibuka kinara kutoka kwa Taasisi mbalimbali zinazohusiana na sekta ya makazi kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika, tuzo za AUHF zinatambua michango thabiti ya kuendelea sekta ya makazi barani Afrika.


"Ushindi wa WHI ulitokana na utekelezaji wake wa kipekee katika kubuni na kutekeleza miradi ya Nyumba yenye gharama Nafuu zaidi na hivyo kuleta unafuu kwa wanunuzi ikiwalenga watumishi wa Umma na wanachama mifuko ya hifadhi ya Jamii"


Aidha, tathmini ilihusisha kuangalia kazi halisi iliyotekelezwa na WHI pamoja na mazungumzo ya moja kwa moja na wanufaika wa miradi yake, hii ilitoa kupata maoni ya moja kwa moja kutoka kwa wananchi waliofaidika  na miradi ya makazi ya WHI ambapo walielezea jinsi njia nafuu za malipo zimewasaidia kufikia ndoto yao kumiliki nyumba.

AUHF ni shirika muhimu linalounganisha wadau makazi barani Afrika kwa zaidi ya miaka 40 linawezesha washiriki wake kuendeleza ufumbuzi zaidi wa makazi ya bei nafuu, aidha tuzo hiyo ni uthibitisho wa dhamira ya Serikali kupitia ofisi ya Rais Menejment ya utumishi wa Umma na utawala bora katika kuwawezesha wananchi wake kupata makazi nafuu

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI