Header Ads Widget

MAKALA:USIMAMIZI NA MFUMO WA ELIMU CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WASI

Na- Nihifadh Abdulla.

Zanzibar :Tathmini iliyofanywa mwezi wa Novemba mwaka 2024 kupitia Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake upande wa Zanzibar TAMWA –ZNZ ambayo ilifanyika kwenye aadhi ya skuli za msingi na sekondari upande wa Unguja  ili kubaini kama wasichana walikuwa wanapewa nafasi za uongozi, hasa nafasi ya Rais .

Ripoti ya utafiti huo inaeleza kuwa matokeo yameonyesha kuwa kati ya skuli za msingi, wasichana 9 walishika nafasi ya Rais kati ya skuli 28, ikiwakilisha asilimia 32. 

Katika skuli za sekondari, skuli nne zilifanyiwa tathmini, na ilionekana kuwa wasichana 7 walishika nafasi ya Rais kati ya skuli 25, sawa na asilimia 28.  

Hafidh Abdi ni Mkurugenzi  wa Jumuiya ya Mazingira Jinsia na Utetezi Pemba-PEGAO amesema ni wakati taasis za kiraia na Serikali zitatengeneze mazingira bora ambayo watamuweza mtoto wa kike aweze kushiriki katika uongozi ngazi za maamuzi  kwa kuwapatia wasichana mafunzo ya uongozi 

“Hii itawasaidia kupata ujuzi wa kuijua jamii yao vizuri, wanajitambua  na wanakuwa na uwezo wa kusimamia changamoto za jamii na hivyo huwa rahisi kupata nafasi hizo baadae”

Amesema Hafidh wakati akizungumza kwenye Mkutano huo. Huku akitaka kuwa ushiriki huo mdogo wa wanawake katika katika uongozi   unatokana na vikwazo mbalimbali ikiwemo vya kimila, utamaduni na dini

 “Katika utafiti huu tumebaini familia zinawakataza wasichana kuwa viongozi kwasababu wao niwanawake, kutokuungwa mkono na wanafunzi pamoja na kukosa elimu ya kujitambua na kujiamini hivyo kushindwa kujitetea”Amemaliza Hafidh.

  

Wapo wanawake ambao walipata nafasi za kuwa viongozi wakiwa wadogo sasa wamepata nafasi ya kuwatetea wengine,Fathiya Mcha Makame ni Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari Kidimni amesema kuwa  nilipopata barua kwamba  nitakuwa mwalimu mkuu nililia mbele ya viongozi. 

“Nikasema siiwezi hiyo nafasi nikaambiwa utaiweza hii imetokana na kukosa elimu ya uongozi huko nyuma”.Amesema Fathiya Mcha Makame huku akiendeleza jukumu la kuwasaidia wanafunzi kuwa viongozi katika ngazi za skuli.

Mkataba wa kikanda wa nchi za kusini mwa Afrika uliotiwa saini mwaka 2008  wenye vifungu 43 unaeleza kuondoa tofauti na  kuwahusisha wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo ili kufikia usawa wa kijinsia.

Kifungu namba 13 kinaeleza kuwekwa mikakati madhubuti ya kuwawezesha wanawake kushiriki katika mchakato mzima wa uchaguzi na upigaji kura na kuondosha mila na desturi potofu zinazopingana na maendeleo ya mwanamke katika siasa na uongozi 

Licha ya jitihada mbalimbali suala linalohusu hadhi ya mtoto wa kike na msichana bado ni kitendawli kutokanana vikwazo mbalimbali vinavyomwandama ambavyo vinakinza lengo na ndoto ya mwanamke kuwa kiongozi,Ali Mussa, ni Afisa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali Idara ya elimu maandalizi na msingi Zanzibar amesema kazi ya kumjenga mtoto wa kike kuwa kiongozi ni kubwa lazima kupatikane nguvu ya pamoja kufikia lengo.

”Tujitahidi kujua kuwa haya masuala yanaanzia nyumbani na ni vyema zaidi kuona kuwa kila mmoja ana nafasi ya kusimamia suala la malezi na lengo la kuwa viongozi” 

Amesema Ali ambaye ameongeza kuwa ndani ya jamii imezoeleka mtoto kuanzia miaka mi nne hupelekwa madrasa huko hufunzwa mwanamke hafai kutoa sauti na kuwa kiongozi hivyo akifika maiaka 10 huwa vigumu kumbadilisha kutokana nakwamba kasha jengewa imani kwa Aya na Hadithi 

“Nitoe wito kwa mashirika ya kiraia ikiwemo TAMWA kushirikiana na Serikali katika kubadilisha mtazamo wa kijamii juu ya elimu ya uongozi wasichana”Amehitimisha.

Amina Juma ni mwanafunzi skuli ya Sekondari Jumbi amesema mtoto  wa kike kuwa kiongozi kuna kuwepo na vikwazo vingi vya kukatishwa tamaa ikiwemo  maneno ya kejeli pindi akijitokeza kugombea.

 “Niwaambie wanafunzi wenzangu tusikate tamaa tuendelee kuzikabili na changamoto zinazotokea na tuzifanye kuwa ni fursa kwetu kufikia lengo” Amesema Amina ambaye ni kiongozi.

Hawra Shamte ni mwakilishi wa Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar JUWAUZA, amesema kuwa changamoto kama unyanyasaji, mtazamo hasi wa kijamii, na kukosa fursa sawa na wavulana zinawafanya wasichana walio wengi ambao wwenye ulemavu kushindwa kufikia malengo yao.

“Changamoto zinazowakabili wasichana wenye ulemavu zinapaswa kuangaliwa na kuwekwa kwenye usawa wa elimu ya uongozi kwa wote kwa mfano hizo serikali za wanafunzi ni nadra kumpata kiongozi mwanamke mwenye ulemavu ni vyema kundi hilo kuangaliwa pia” Hawra amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania upanda wa Zanzibar TAMWA Dkt Mzuri Issa  amesema kuwa masuala ya mahitaji ya kijinsia ni ya kimkakati na yana umuhimu mkubwa zaidi katika jamii. 

“Usawa wa kijinsia lazima uanze mapema kwenye elimu ya wasichana zamani watoto wa kike hawakupelekwa skuli walianza kupelekwa 1960 hii imekuja kwa mkakati maalum na manufaa yake yanaonekanwa kwa sasa 

”Amesema ili kufanikiwa zaidi lazima kuwafundisha wasichana kudai haki zao wenyewe kupitia mbinu mbalimbali na kujua uongozi ni kitu gani kuanzia skuli za msingi,sekondari vyuo pamoja na  madrasa.

”Hii itawajenga na siku za mbele tutakuwa na viongozi wa kike madhubuti ambao wamezoea kuongoza na kuwa majasiri” Amemaliza Dkt Mzuri Issa.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI