Header Ads Widget

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA MAADHIMISHO YA SIKU YA FIMBO NYEUPE


Na Esther Machangu, Moshi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 25, 2024 amewasili mkoani Kilimanjaro ambapo anamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Fimbo Nyeupe na Miaka 60 ya Chama cha Wasioona Tanzania (TLB).

Katika hatuba yake waziri Mkuu amewataka  wazazi kutokawaficha watoto wenye ulemavu ili wapatiwe elimu ya pamoja na kuwa huru na kujumuika na watoto wenzie.

Hata hivyo majaliwa amewataka walemavu hao kujiunga kwa vikundi ili wapate mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri zote nchini.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amewahakikishia kutatua changamoto ya walemavu hao kupatiwa ofisi katika mkoa huu.

Siki ya Kimataifa ya Fimbo Nyeupe huadhimishwa kila Oktoba 15 kwa lengo la Kuelimisha jamii kuhusu haki na uwezo wa watu wenye ulemavu wa kuona, Kutambua umuhimu wa fimbo nyeupe katika kusaidia watu wenye ulemavu wa kuona kusafiri kwa usalama na uhuru na hatimaye kufikia malengo yao.

Aidha, Siku hiyo pia ina lengo la kuhamasisha ujumuishaji wa watu wenye ulemavu wa kuona katika jamii na kuhakikisha wanapata fursa sawa katika elimu, ajira, na huduma zote nyingine.

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Upatikanaji wa Teknolojia Saidizi na Fikivu ni Mkombozi kwa Uchumi Endelevu kwa Mtanzania asiyeona.”

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI