NA,Jusline Marco;Arusha
Mwenyekiti wajumuiya ya Wazazi Mkoa wa Arusha Ezron Mbisse amewataka Wazazi na walezi kuwakumbuka watoto wakiume na kutoa kipaumbele kwao sawa kama wanavyotoa kwa watoto wakike.
Ezron ametoa wito huo alipokuwa mgeni Rasmi Katika mahafali ya kwanza ya kidato Cha nne ya shule ya sekondari Naurei Golden Soilis iliyopo Kata ya Nkwamrua Wilayani Arumeru Mkoani Arusha ambapo mahafali hayo yamekwenda sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumbanvya madsrasa ya shule hiyo.
Ameongeza kuwa atahakikisha anafikisha ombi la shule hiyo kutumia nishati mbadala Kwa uongozi waserikalini Ili shule hiyo uanze kutumia nishati safi ya kupikiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule hiyo ya Naurei Golden Soilis Stiven Ndosi amesema kuwa Wanajitaji zaidi ya shilingi milioni 80 Ili kukamilisha ujenzi wa madsrasa mawili... voice
Naye Mkuu wa shule naurei Golden Soil anaitwa Tito Kaaya amesema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 2021 ikiwa na wanafunzi 28 na baadaye idadi ikiongezeka na Kwa Sasa ina wanafunzi 110 huku wanafunzi wanaotarajia kuhitimu kidato Cha nne wakiwa 32.
Ameongeza kuwa shule hiyo mpya imeshiriki mitihani ya kitaifa kidato Cha pili mara mbili nakuwa na ufaulu wa daraja la kwanza na la pili tuu ambapo ilishika nafasi za juu kitaifa na matarajio Yao Kwa Sasa ni ufaulu wa Daraja la kwanza tuu Kwa kidato Cha nne mwaka huu.
0 Comments