Na Matukio Daima Media App,
KISA Lauden mkazi wa Ghana Jijini Mbeya mama wa watoto watano amesema kuwa baada ya kuingizwa kwenye mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF )maisha yake yamebadilika kwa familia yake kula milo miwili baada ya mlo mmoja wa awali kwa siku huku wakilala kwenye mkeka.
Bi.Lauden amesema kwamba changamoto za kimaisha alianza kuzipata baada ya mume wake kumtelekeza baada ya kukataa kutoa mimba yake ya tano na hivyo kumuacha akiteseka na watoto na kutokomea kusikojulikana tangu mwaka 2006 mpaka sasa.
Akizungumza na Matukio Daima Media October 24,2024 jinsi TASAF ilivyoweza kumwinua kimaisha na familia yake ,Kisa Lauden amesema kuwa baada ya Kuonwa na mfuko huo maisha yake imekuwa miujiza kwani yamekuwa na mabadiliko .
"Hali yangu ya kimaisha niliyokuwa nayo kipindi hicho ilikuwa ni ngumu kulisha watoto ilikuwa ni ngumu watoto kupata chakula pamoja kusomesha yaan ilikuwa changamoto wakila.mlo mmoja ambayo ni mchana basi mpaka kesho yake,mume wangu tuliachana mwaka 2006 kwa hiyo kusomesha watoto juu yangu kula watoto ,mavazi vyote ilikuwa kupitia TASAF na nilipoingizwa kwenye mfumo huu nilishukuru nimeona matunda yake kwani serikali imekuwa msaada mkubwa"amesema.
Akielezea zaidi amesema kuwa viongozi wa TASAF walishauri kutengeneza vikundi na kusema fedha wanayopewa wasile yote bali wanunue mahitaji ya watoto , kununua chakula na kufanya biashara ambayo itakuwa mkombozi kwao katika kujiinua kiuchumi.
Meleckzedeck Nduye Ofisa Habari wa mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) amesema kuwa moja ya marshati ambayo wanawapa wanufaika wa mfuko huo ni kuhakikisha fedha hizo zinawanuisha kama kaya ili waweze kuinua uchumi wao na kuondokana na dibwi la umasikini uliokithiri ambao waliwakuta nao.
"Sasa hivi tunazungumza zaidi ya miaka miaka nane ( 8 )toka tumeanza uhamilishaji wa fedha hizi kwa walengwa na tumeona matokeo makubwa walengwa wetu wengi walikuwa na hali mbaya lakini sasa wanaweza kusimama wenyewe kwa miguu yako na wanapata milo mitatu wanaweza kuja kwenye matukio makubwa ya kitaifa kama haya na kuonyesha vitu ambavyo wanafanya katika hali halisi isingekuwa kawaida lakini kazi ni njema kwani walengwa wanafanya vitu vinavyoonekana ambavyo vinatokana na kazi ya mikono yenu"amesema Ofisa Habari huyo.
Aidha Nduye amesema kuwa siri ya mafinikio kwa walengwa ni TASAF kuwapa elimu ya umoja ,kujiunga kwenye vikundi,elimu ya kuweka na kukopa ambayo inasaidia kukua kwa haraka na kufanya vitu vikubwa kwa wakati mmoja.
Mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF)upo kwenye maadhimisho ya huduma za fedha kitaifa ambayo yalianza October 21,2024 na yatahitimishwa October 26 mwaka huu.
0 Comments