Header Ads Widget

WANANCHI WATAKIWA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI WAKATI WAKUCHAGUA VIONGOZI



Na Fatma Ally, Matukio Daima App


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na uratibu William Lukuvi amewataka wananchi kufanya maamuzi sahihi katika kuwachagua viongozi ambao watakwenda kufanyakazi na Rais Dkt Samia Suluhu za kuwaletea wananchi maendeleo katika mitaa yao.


Wito huo ameutoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungumza na wananchi wa Kata ya Pugu mtaa wa Bangulo mara baada ya kukagua miradi ya maendeleo mikubwa iliyopo katika Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam katika Jimbo la Segerea, Ukonga na Ilala.


Waziri Lukuvi awali alikagua na kuzindua miradi mitatu ya maendeleo katika majimbo hayo ambapo katika Jimbo la ilala amekagua ujenzi wa barabara ya Tukuyu, Jimbo la Segerea amezindua na kuweka jiwe la msingi katika shule ya Sekondari Liwiti na Jimbo la Ukonga amekagua Tanki kubwa la maji.


"Lengo leo ni kuja kuonana na wananchi pamoja na kuangalia mafanikio makubwa ambayo yamefanywa na Rais Dkt Samia chini ya Serikali ya CCM naamini wananchi hamutofanya makosa wapimeni viongozi watakaokuja kugombea kwa hoja na sio mihemko ili mupate maendeleo"



Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema wanatarajia kupokea zaidi ya  Shilingi Bilioni 302 kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Barabara Wilayani humo.


Amesema, wamesha pokea shill Bill 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Liwiti ambayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu William Lukuvi ameweka jiwe la msingi kwenye shule hiyo ambayo imejengwa na Serikali kupitia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.


"Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani hapa ni kutokana na ushirikiano wa viongozi walipo jijini hapa katika kuhakikisha wanatimiza adhma ya  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kutatua changamoto zinazo wakabili Wananchi" amesema  DC Mpogolo.


Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Pugu Stetion Mussa Shaban ameishukuru Serikali kwa kuwatatulia changamoto kubwa ya maji na Barabara ambayo ilikua ni kikwazo kwao jambo ambalo litachangia katika harakati za maendeleo katika ujenzi wa taifa.


"Serikali ya awamu ya sita sisi wanaBangulo imetutendea makubwa sana tulikua na changamoto ya maji lakini tunaishukuru Serikali imetujengea tenki kubwa, imewekeza bill 36.7 na tunasubiri Barabara zetu zijengwe Kwa kiwango Cha lami naamini wananchi hawatafaya makosa kwenye uchaguzi"




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI