Header Ads Widget

WANA HABARI KAGERA WAPATA PA KUZISEMEA CHANGAMOTO ZAO

 


Na Shemsa Mussa.

Ni baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa kuzitembelea Ofisi za waandishi wa habari Mkoa wa Kagera lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua kero zao ikiwa ni mwendelezo wa kusikiliza kero za wadau mbali mbali wa Mkoa huo.

RC Mwassa amezitembelea Ofisi za waandishi wa habari Mkoani Kagera   zijulikanazo kama  Kagera Press Club(KPC) zilizopo Manispaa ya Bukoba (Bohari)

RC Mwassa alizungumza na waandishi hao masula mbali mbali ya maendeleo  yahusuyo Mkoa huo na kisha  nakuwapa nafasi waandishi hao ili nao waeleze waliyonayo .

Kubwa zaidi kwa waandishi hao lilikuwa ni kuomba ushirikiano kati ya Ofisi yake ili waweze kufanya kazi yao kwa urahisi pamoja na kuomba kupanuliwa kwa Ofisi zao na kuongezewa baadhi ya vifaa mbali mbali vitakavyowezesha kufanikisha kazi zao.

Mmojawapo wa wanahabari hao 
aliyejulikana kwa jina la Benson Eustace alimpongeza Mkuu huyo wa Mkoa kwa ujio wake katika ofisi hizo huku akijivunia kuona Mkuu huyo anakuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza  kuwatembelea waandishi wa habari Ofisini kwao.

"Mimi na wenzangu tunayofuraha kubwa Mhe, kukukaribisha hapa kwetu kwani umekuwa  Mkuu wa Mkoa wa kwanza kufika hapa Viongozi wengine tumekuwa tukikutana nao katika kazi bila wao kujua wapi zilipo Ofisi zetu" alisema Benson.

Benson aliongeza kuwa wapo wanachama wa Chama hicho zaidi ya 60 na kuwa Chama hicho kimekuwa mwavuli wa kuwalea waandishi wa habari huku akieleza matakwa yao kwa ujumla kuwa ni pamoja na kuomba ushirikiano mkubwa kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa ili kupata habari, kumuomba kiongozi huyo kuwalea na kuwakuza Vijana kitaaluma na kiuchumi katika mkoa huo.

Akijibu hoja na changamoto za waandishi hao RC Mwassa alisema atajitahidi kuwafikia Vijana ikiwa ataanza na kuwapatia sehemu nyingine ya Ofisi na baadhi ya vifaa, kuwapatia semina ya taaluma ya uandishi itakayoendeshwa na wataalamu wabobezi kutoka Kagera na nje ya Kagera ili kuwapiga msasa na kuwaongezea ujuzi zaidi ikiwa ni kuandika habari za maendeleo, namna ya kuandika habari za uchaguzi.

"Maisha ya waandishi nayajua sana ningetamani kuona mwandishi wa habari Kagera analipwa vizuri akifanya kazi nitakuwa wa kwanza kuwatetea"alisema Hajat Mwassa

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka waandishi hao ambao bado hawajajiunga na umoja huo kujiunga na hata kwa makundi mengine ya ki habari ili kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo kusoma,kupata nafasi ya kuudhuria mikutano mikubwa nje ya Mkoa ili kunufaika na taaluma hiyo huku akivipongeza vyombo vya habari Mkoani humo hasa redio za kijamii kwa namna zinavyohabarisha umma.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI