Na Matukio Daima App.
WAKULIMA Wawezeshaji wilaya ya Bunda Mkoani Mara, wamekabidhiwa Baiskeli na Bodi ya Pamba ili waweze kuwafikia na kuwapa Elimu ya Kilimo bora cha pamba wakulima wa pamba katika vijiji vya Halmashauri ya Mji wa Bunda na wilaya.
Katika taarifa iliyotolewa na Bodi ya Pamba kwa Umma, imeeleza kuwa wakulima wawezeshaji wanafanya kazi kwa ukaribu na Maafisa Ugani ngazi ya kata na vijiji, ili kuhakikisha wanafikisha Elimu ya kanuni 10 za kilimo cha Pamba kwa wakulima.
Imedaiwa kuwa wilaya ya Bunda ina jumla ya wakulima wawezeshaji 107 na kati yao 78 wamepokea baiskeli zilizotolewa na serikali kupitia Bodi ya Pamba.
Aidha kutumia wakulima wawezeshaji ni miongoni mwa mkakati wa Bodi ya Pamba kuboresha utoaji wa huduma Bora za Ugani Kwa wakulima Kwa lengo la kufikia tani 1,000,000 ifikapo ifikapo msimu wa 2025/2026.
Hata hivyo jumla ya wakulima wawezeshaji wa pamba 5200 wametambuliwa nchi nzima, na baiskeli 2500 zimetolewa kwa wakulima wawezeshaji ambao ni wawiliwawili kwa kila kijiji katika mwaka wa fedha 2024/2025.
0 Comments