Na Hamida Ramadhan matukio Daima app DODOMA
BARAZA Kuu la Mtandao wa usimamizi wa rasilimali watu katika sekta ya umma (APS-HRMnet ),inatarajia kuwakutanisha pamoja Mawaziri wa Sekta ya Umma, Makatibu Wakuu, Wasimamizi wa Rasilimali Watu, watunga sera, wasomi, na wataalamu kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika kwa ajili ya mijadala na juhudi za pamoja.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lakini pia APS-HRMne Rais wa mtandao wa APS-HRMnet Xavier Daudi, Wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mtumba kuhusu mkutano wa 9 wa APS-HRMnet .
Amesema Jumuiya hiyo inayolenga kuendeleza taaluma ya usimamizi wa rasilimali watu katika Utumishi wa Umma ili kuhakikisha utoaji huduma bora kwa wananchi ilipendekezwa kuundwa kutokana na mapendekezo ya Mkutano wa 29 wa Jumuiya ya Usimamizi wa Utumishi wa Umma wa Afrika (AAPAM) uliofanyika Mbabane, Swaziland mnamo Septemba 2007.
"Mnamo tarehe 26 Februari, 2009, Mawaziri wanaohusika na Utumishi wa Umma Barani Afrika, Wasimamizi wa Rasilimali Watu katika Sekta ya Umma, Taasisi za Maendeleo ya Menejimenti, pamoja na wanachama wa Jumuiya ya Usimamizi wa Umma wa Afrika walikusanyika Arusha, Tanzania na kuunda APS-HRMnet kwa kupitisha Katiba ya Afrika, " Alisema .
Na kuongeza "Juhudi hii ililenga kutambua umuhimu wa ushirikiano na mtandao miongoni mwa taasisi za sekta ya umma za Afrika katika masuala ya utetezi, maendeleo ya kitaalamu ya usimamizi wa rasilimali watu, na ushirikishwaji wa taarifa na maarifa kwa ajili ya ufanisi katika Sekta ya Umma, " Amesema Naibu Katibu Mkuu huyo.
Aidha amesema APS-HRMnet iliundwa kwa lengo la kutafsiri mikakati ya maendeleo ya kitaifa, kikanda, na kimataifa kuwa matokeo halisi kwa kuwapa mamlaka rasilimali watu wenye uwezo.
Hata hivyo ameeleza Nchi wanachama zinajumuisha kanda tano za Afrika, ambazo ni; Afrika Magharibi, Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, Afrika Kaskazini, na Afrika Kusini.
"Tanzania ikiwa ni mojawapo ya nchi wanachama wa APS-HRMnet imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 9 wa APS-HRMnet ambao utafanyika tarehe 4-7 Novemba 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) huko Arusha.
Ameelezea malengo mahusisi ya APS-HRMnet kuwa ni Kukuza ubora, uadilifu, na viwango vya kitaaluma katika usimamizi wa rasilimali watu katika sekta ya umma barani Afrika.,Kutambua na kushiriki mbinu bora za usimamizi wa rasilimali watu ,
Kuwapatia wataalamu wa usimamizi wa rasilimali watu katika sekta ya umma barani Afrika zana, mifano, stadi, mbinu, na data za kuboresha ufanisi wa mipango yao,Kukuza ujifunzaji endelevu, kuongeza maarifa, kuboresha ujuzi, na kuendeleza kizazi cha sasa na kijacho cha wataalamu na viongozi wa usimamizi wa rasilimali watu katika sekta ya umma barani Afrika.
Kusaidia na kutetea nafasi ya kimkakati ya wasimamizi wa rasilimali watu kama washirika muhimu na wa msingi katika upangaji na usimamizi wa maendeleo na mabadiliko katika sekta ya umma,Kusaidia juhudi za bara na kikanda barani Afrika katika kutekeleza ahadi za utumishi wa umma zinazofanana, kama vile Mkataba wa Utumishi wa Umma Afrika.
Hata hivyo Mkutano wa 9 wa Mwaka unaongozwa na kaulimbiu: Utawala Imara na Ubunifu: Kujenga Sekta ya Umma Yenye Mwelekeo wa Baadaye Kupitia Uongozi wa Rasilimali Watu.
Hivyo basi Kupitia mkutano huu, APS-HRMnet inalenga kujenga sekta ya umma inayoweza kukabiliana na mabadiliko na kutoa majibu yanayokidhi mahitaji ya wananchi kwa njia endelevu.
0 Comments