MWENYEKITI wa Baraza la Vijana Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Ngara, Titho Philimon na Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) wilayani hapa, Catherine James wamejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) na kupokewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho taifa, Mohamed Kawaida.
Wakizungumza wakati wa kuhama chama hicho juzi, viongozi hao walidai walifikia uamuzi huo kutokana na kuwa katika chama chao bila maendeleo yoyote.
Mwenyekiti wa BAVICHA, Philimon alisema aliamua kwenda CCM baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan na kuwa hatua hiyo itamuwezesha kuungana na vijana wenzake wa kitanzania zaidi ya milioni 21.3 ili kufikia chachu ya maendeleo.
Mwenyekiti BAWACHA Wilaya, Catherine alisema amekuwa kiongozi wa chama hicho kwa miaka 20, lakini haoni mafanikio ndani ya chama hicho.
@Nipashe
0 Comments