Header Ads Widget

VIONGOZI JESHI LA POLISI JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI EAC WAKUTANA NA KUJADILI UHALIFU WA MITANDAO

Na Fatma Ally Matukio DaimaApp Dar 

VIONGOZI wa Jeshi la Polisi kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki EAC leo wamekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kueka mikakati madhubuti ya kukabiliana na kupambana na matukio ya uhalifu wa mitandao ambao umevuka mipaka na viashiria vya ugaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai DCI Ramadhani Kingai wakati akimuwakilisha Kamishna Jeneral wa Polisi IGP Camillius Wambura katika mkutano wa 8 ambao umeshirikisha nchi 6amesema kuwa viongozi hao wamekutana kwa lengo la kubadilishana uzoefu namna ya kukabiliana na matukio ya uhalifu.

Amesema kuwa, jumuiya hiyo itahakikisha inaweka mikakati ya kupambana na uhalifu uliovuka mipaka ikiwemo usafirishaji binadamu,dawa za kulevya,ugaidi na hualifu wa mitandao pamoja na kubadilisha uzoefu hasa kwa wenzao wanefanikiwa.

"Wakuu wa kijeshi wamekutana kujadili mambo mbalimbali ikiwemo uhalifu, ugaidi, uhalifu uliovuka mipaka nchi ili kuhakikisha ardhi ya Afrika inakua salama,tutahakikisha tunawashughulikia wahalifu mpaka sasa tupo salama"amesema DCI Kingai

Amesema kuwa, kwa Afrika Mashariki uhalifu mkubwa ni wa ni mitandaoni na viashiria vya ugaidi, huo ni uhalifu mpya kutumia mitandao, kwani zamani mtu alikua anafika benki na bunduki kwenda kufanya uhalifu wa wizi lakini kwa sasa mtu anatumia simu kufanya uhalifu.

"Tulipofikia inabidi tujifunze mbinu mpya za kukabiliana na wahalifu ili kuhakikisha wananchi na nchi inakua hasa hasa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki  kwani mtu anaweza akawa yupo Kenya lakini akaiba pesa kutoka benki ya Tanzania," 

Sambamba na hayo amesema Tanzania ni moja ya nchi inayoshirikiana na nchi nyingine ili kuweza kusaidia ardhi ya Afrika Mashariki inakuwa salama ambapo mpaka sasa wamekuwa wakibadilishana taarifa za wahalifu kupitia mtandao na wengine wamekamatwa na kuweza kudhibitiwa.

"Jumuiya yetu ni budi kuimarisha miundombinu ya usalama na kubadilishana taarifa kwani tunatambua changaomto kubwa Uhalifu wa mitandaoni na Vishiria vya ugaidi ndiyo shida inayotusumbua hivyo nchi moja haiwezi peke yake kulabiliana lazima kuwepo na mashirikiano na mikakati ya pamoja" amesema DCI Kingai.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI