Header Ads Widget

TET, KOREA WASHIRIKIANA KATIKA TEHAMA NA MICHEZO SHULE YA SEKONDARI KIMARA







TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imeambatana na Wadau kutoka Korea Kusini Metropolitan na Wanafunzi Viongozi [Global Leaders] kutoka  Gwangju wametembelea na kufanya mashirikiano pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kimara, ilipo Manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam.

Katika tukio hilo mapema leo Oktoba 21,2024, Wanafunzi hao Wakitanzania na Korea waliweza kubadilisha ujuzi ikiwemo masuala ya michezo na masomo.

Ambapo kwa pamoja waliweza kuonesha ujuzi katika michezo, Ngoma za kikorea na kitanzania, Sanaa ya mapigano ya Taikondo na baadae walijumuika katika kuunda magari ya watoto yanaotumia mfumo maalum wa 'Infrared', ambapo walijifunza na kuunda magari hayo.

Awali Afisa Utumishi mwandamizi kutoka TET, Bw. Elias Kabate aliyeambata na baadhi ya wakuza Mitaala kutoka TET amesema kuwa, ushirikiano huo ni  mahusiano mazuri yaliopo baina ya Tanzania na Korea katika sekta ya elimu hapa nchini ambapo Wanafunzi zaidi ya 35 kutoka Korea wanapata kutembelea katika baadhi ya shule nchini na kujifunza masuala mbalimbali.

Kwa upande wake, Mkuu wa msafara wa wanafunzi hao kutoka Korea, Bw. Lim Dong Youn ameishukuru Serikali ya Tanzania ambapo ameahidi kuendelea kutoa mashirikiano zaidi katika masuala ya TEHAMA na kujifunza tamaduni za pande zote mbili kupitia mpango  huo wa Wanafunzi viongozi wa Korea Gwangju kutembelea Tanzania.

Nae, Afisa Elimu Takwimu Sekondari Manisapaa ya Ubungo, Bi.Zania Kesowani akizungumza na Wanafunzi wa Sekondari Kimara wakati wa kutoa neno la Shukrani kwa wageni hao, ameishukuru Serikali ya Korea Kusini na huku pia akiwaomba Wanafunzi kuendelea kuyatunza madarasa ya TEHAMA ilikuweza kujifunza Masoko ya Sayansi na teknolojia.

Aidha, Ugeni huo wa Korea unatarajiwa kutembelea shule ya Wasichana Dar es Salaam (Dar es salaam Girls)  iliyopo Mbezi Luguluni katika Halmashauri ya Manisapaa ya Ubungo lengo kuendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia ya Tehama katika ufundishaji na ujifunzaji.




















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI