Header Ads Widget

TCRA KANDA YA KASKAZINI YAZINDUA KAMPENI YA "NI RAHISI SANA"

NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Mamlaka ya mwasiliano Tanzania (TCRA) kanda ya kaskazini imezindua kampeni ya "NI RAHISI SANA" yenye lengo kuwahimiza watanzania kujilinda dhidi ya uhalifu mtandaoni kutokana na watu wengi kutokuwa na ujuzi wa kutosha wa matumizi sahihi yq mitqndao ya kijamii.

                          

Akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha Octoba 9,2024 Meneja wa TCRA kanda ya kaskazini Mhandisi Fransis Mihayo alisema kuwa uwezo wa mazingira salama mtandaoni yatawezesha kufikia malengo ya uchumi wa kidijiti kwani matumizi ya teknolojia yamekuwa yakiongezeka kwa kasi na ni muhimu katika maisha ya kila siku.

" Kutokuwa na ujuzi wa kutosha wa matumizi ya mitandao ya kijamii pamoja na kulinda uswlama wao mtandaoni ni jambo linalowafanya kuwa hatarini kwa mashambulizi, ulaghai wa mtandaoni na kuwa na matumizi mabaya," Alisema Mhandisi Mihayo.

Aidha alifafanua kuwa TCRA inatambua umuhimu wa kukuza elimu ya kidigitali na usalama mtandaoni ili kuhakikisha mazingira ya kidigitali yana usalama na kuhamasisha fursa zilizopo kwa kishiriki kwa usalama kiuchumi na kisiasa hasa kipindi cha chaguzi mbalimbali.

"Mabadiliko ya kasi ya teknolojia yamekuwa  yakienda sambamba na ongezeko la vitendo vya kiulaghai mtandaoni ambapo  wahusika wamekuwa wakibuni mbinu mpya kila wakati na kusababisha elimu ya usalama iwe endelevu kwa jamii nzima," Alieleza.

Alifafanua kuwa kampeni hiyo itakayodumu kwa miezi 6 itawalenga zaidi watoto,vijana, wazee, watu wenye mahitaji maalum, mashirika, wanafunzi, wafanyabiashara, watoa maamuzi pamaja na mashirika ya kitaaluma ambapo itatolewa kupitia vyombo vya habari, stend za mabasi, minadani pamoja na ujumbe kwenye simu za mkononi.

Hata hivyo alisema kuwa baada ya kutekeleza kampeni hiyo itaongeza uelewa kwa umma juu ya kutosambaza taarifa za uongo, kugundua maudhui ya upotoshaji pamoja na kuongeza idadi ya watumiaji na mwingiliano kupitia mitandao ya kijamii

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI