Na Esther Machangu,
Jamii imeaswa kutumia mbegu za asili katika Kilimo ili kupata mazao bora na yenye virutubisho vya kutosha.
Hayo yameelezwa leo October 16,2024 wakati wa mafunzo ya vijana yalitolewa na shirika la Tanzania Youth Coalition(TYC)
Akitoa mafunzo ya Kilimo na mabadiliko ya Tabia nchi mwezeshaji katika mafunzo hayo Joseph Mfanga kutoka mtandao wa vikundi vya wakulima na wafugaji Mkoa wa Kilimanjaro (MVIWAKI) amesema wamejikita katika kuhakikisha vijana wanatambua umuhimu wa kilimo ekolojia, ubora wa mbegu za asili katika kutoa chakula bora Chenye virutubisho vyote na ustahamilivu wa mbegu hizo katika kuhimili ukame.
Mfanga ameongeza kuwa mbegu asilia zimekuwa kichocheo kikubwa cha upatikani chakula bora ambacho kitawaepusha watu wengi kupata mgonjwa yanayotokana na ulaji wa vyakula vya kiwandani.
Wakizungumza katika mafunzo hayo Baadhi ya vijana hao akiwemo Straton Lyimo na Lidya Sakaya wamesema ikiwa vijana wata tambua umuhimu wa mbegu za asili na faida zake itakuwa rahisi kwa jamii kubadilisha mtazamo wa kuwa mbegu hizo hazina mazao ya kutosha na pia itasaidia kwa kizazi kijacho kuendeleza matumizi ya mbegu hizo.Naye Lusila Chima afisa Maendeleo vijana Wilaya ya Hai amewatoa hofu vijana wanaotaka kufanya shughuli za ujasiriamali, kilimo pamoja ufugaji wasisite kuanzisha shughuli zao kwani Serikali ya awamu ya sita chini ya uwongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan wametoa mikopo ya Halmshauri zote nchini ili kuwawezesha vijana, akina mama, na watu wenye ulemavu kunufaika na mikopo hiyo.
Hata hivyo Afisa Miradi kutoka Tasisi hiyo isiyokuwa ya kiserikali Tanzania youth Coalition (TYC) Josephine Onesmo amesema tasisi hiyo inalenga kumjengea uwezo kijana ili aweze kushiriki katika mambo mbalimbali ya kijamii ambapo katika mafunzo hayo waliyoyatoa kwa vijana hao yatakuwa chachu kwa vijana hao kuanza kuitazama Sekta ya kilimo kwa wigo mpana hasa kujikita kufanya kilimo asilia na utunzaji wa mbegu za asili.
0 Comments