NA ANDREW CHALE, MATUKIO DAIMA APP, DAR.
MWIGIZAJI Mkongwe Yusufu Kaimu maarufu kama Mzee Pembe ambaye alikuwa akiigiza na rungu katika video zake na michezo mbalimbali ya maigizo amefariki dunia siku ya leo Oktoba 20,2024.
Kwa mujibu wa mmoja wa Waigizaji, msanii Mkono Mkonole amezungumza na Matukio Daima App amesema wamepata pigo kubwa, kwa kuondokewa na Mzee Pembe.
"Mzee wetu ametutoka na tunatarajia kumpumzisha Jumatatu Oktoba 21,2024 katika makaburi ya Yombo Chama.
Msiba upo nyumbani kwake hapa hapa Yombo Chama, Ndugu jamaa na marafiki na wadau wote tunaweza kufika katika kumsindikiza mwenzetu " Amesema Mkono Mkonole.
Wasanii mbalimbali wametoa salamu za pole kupitia katika Akaunti zao za mitandao ya kijamii Waigizaji wenzake akiwemo Ray Kigosi, Tin White kwa nyakati tofauti wameweza kumuomboleza.
Mwenyezi Mungu apumzishe roho yake Mahali pema peponi.
0 Comments