Na, Matukio daima App
SHULE ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere imeingia makubaliano kwa mara ya pili ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Renmin katika nyanja za mbalimbali zikiwemo za mafunzo utafiti na kubadilishana wataalamu.
Wakisaini makubaliano hayo kati ya Mkuu wa Shule ya Mwalimu Nyerere Profesa Marcellina Chijoriga na kiongozi Mkuu wa Chama Tawala Cha China Cha (CPC) kwenye chuo cha Renmin Zhang Donggang katika Shule hiyo iliyopo Kibaha Mkoani Pwani huku wakishuhudiwa na wakufunzi wa vyuo mbalimbali nchini na Wakufunzi wa vyuo kutoka China.
Profesa Chijoriga alisema kuwa makubaliano hayo yatakuwa ni kwa ajili ya kubadilishana wataalamu ambapo wao watakuja huku na wa Tanzania watakwenda kwao ikiwa ni sehemu ya kubadilishana uzoefu.
“Chuo hicho ni kikubwa sana na cha muda mrefu na kiko vizuri kwenye masuala ya utafiti wa uandishi wa vitabu na katika masuala ya uandishi wa vitabu ambapo ushirikiano huo utakuwa na manufaa makubwa sana kwa pande zote mbili,”alisema Chijoriga.
Alisema kuwa chuo hicho cha Renmin kinauwezo mkubwa wa kuwajengea uwezo viongozi wa chama na serikali kwani kiko vizuri sana katika ufundishaji masuala hayo na watatumia uzoefu ili kujifunza kupitia kwao kwani kimeanza muda mrefu.
“Faida hiyo ni kwa vyama sita vya ukombozi Kusini mwa Afrika ambapo China ni msaidizi mzuri kwani wamesaidia ujenzi wa shule hiyo ambavyo ni CCM, FRELIMO, SWAPO, ANC na ZANU-PF msaada kutoka chama cha ukomunisti cha nchini China CPC” alisema .
Aidha alisema kuwa chuo hicho kilichopo Beijeng China kilianza ushirikiano mwaka jana ambapo uongozi wa Shule walikwenda na katibu mkuu wa CCM wakati ule Chongolo na sasa imeanza safari mpya kwa kusaini mikataba hiyo kwani kina uzoefu mkubwa nani cha zamani sana.
“Tunashukuru sana kwani wametuonyesha ushirikiano mkubwa na makubaliano ya kutengeneza ushirikiano huu ni sasa safari mpya imeanz na leo waametupa vitabu tunawashukuru kwani maktaba yetu sasa itakuwa na vitabu vingi na wasomaji wataweza kujifunza masuala mbalimbali ya nchi ya China,”alisema Chijoriga.
"Tumeingia makubaliano katika nyanja za kubadilishana viongozi kwenda kuwa wakufunzi na kubadilishana uzoefu katika mafunzo yatakayofanyika kati nchi hizi mbili tayari Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Palamagamba Kabudi amekwenda China na kutuwakilisha, amesema Prof. Chijoriga.
" Tutashirikiana na China katika nyanja za tafiti mbalimbali kwa sababu hawa wenzetu wako mahiri zaidi kwenye tafiti mbalimbali" amesema Chojoriga.
Kwa kupitia mkataba huu tumekubalia kuwa tutawajengea uwezo viongozi wa chama na serikali pia ikumbukwe hii ni faida kwa vyama sita rafiki vya ukombozi Kusini mwa Bara la Afrika .
Aidha Prof.Chijoriga ametoa shukrani kwa serikali ya China kwa kutoa msaada wa maktaba Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere ambayo imewaongezea thamani huku akisema kuwa wakati umefika wa nchi navyama rafiki kujifunza kwa wenzetu.
Naye alisema Dk Evaristo Haule Naibu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere alisema kuwa China imefanikiwa na tumeona namna gani kutumia njia ili kuona wao wamefanyaje na kufikia hatua kubwa kiasi hicho kwenye maendeleo na CPC inavyotoa dira kuongoza nchi yao wanataka twende pamoja katika miradi yao mikubwa ya kidunia.
Dr. Haule alisema ili kwenda pamoja hivi karibuni Rais Dk Samia Suluhu Hassan alienda China kwenye mkutano wa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika wao wana dira na kufanya kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu ya kazi na watu wawe na uzalendo wa nchi watu wanaangalia changamoto badala ya kuangalia fursa zilizopo.
Naye Dk Theresia Dominick kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akizungumza kwa niaba ya Wakufunzi Mkufunzi wa Shule ya Mwalimu Julius Nyerere.
Dkt.Theresia Dominic amesema kuwa kupitia wenzetu wachina tujifunze kuwa na nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii,"mchina ana nidhamu ya juu katika utendaji wake wa kazi kadhalika wanatabia ya kuzingatia chakula kwa sababu wanaamini katika kulinda afya zao kwa kuzingatia faida ya chakula anachokula je kina faida gani ama kitamletea madhara gani tofauti na sisi ambao huwa tunakula tu ilimladi tumbo lijae"
Ameongeza kwa kusema kuwa watanzania tunapaswa kuwa na nidhamu ya fedha kwa sababu wachina hawana tabia ya ufujaji wa fedha hata kama anazo huwezi kumuona ama kumkuta anabadili mwenendo wa maisha yake" amesema Dkt.Theresia Dominic.
Alisema kuwa badhi ya wafanyabiashara Watanzania wamekuwa wakienda China hivyo wanapaswa kujifunza tabia za Wachina za kufanya kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu ya jambo kwani wanalolifanya Wachina duniani ni mfano wa kuigwa.
Naye kiongozi huyo Zhang Donggang alisema kuwa ushirikiano uliopo baina ya China na Tanzania na nchi nyingine ni katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ambapo wao wanaangalia sana maslahi ya wananchi.
Donggang alisema kuwa nchi za Afrika na China zinapaswa kushikana mkono katika kuhakikisha zinapiga hatua katika masuala ya kimaendeleoili kudumisha umoja uliopo kwani umoja uliopo umeleta mafanikio makubwa.
0 Comments