SERIKALI imeanza kutekeleza Mradi wa kimkakati wa Utafiti wa Mafuta katika Bonde la Eyasi Wembere kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) chini ya Wizara ya Nishati.
Utafiti huo ambao unaofanyika katika wilaya za Meatu Mkoani Simiyu, Mkarama (Singida) na wilaya za Karatu na Ngorongoro (Arusha) umeanza kufanyika kutumia teknolojia za kisasa kupitia wataalamu wa ndani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Msimamizi wa Mradi wa Utafiti wa Mafuta na Gesi katika hilo, Sindi Maduhu amesema Mradi huo unatekelezwa ili kutafuta mafuta na Gesi katika Bonde hilo lenye viashiria vya uwepo wa Mafuta n la Gesi Asilia.
Amesema Bonde la Eyasi Wembere liko katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki na kwamba Bonde hilo linashabihiana na mabonde mengine ya Afrika Mashariki katika nchi za Kenya na Uganda.
Ameeleza kuwa Utafiti wa Mafuta katika eneo hilo ulianza mwaka 2015 ukidhaminiwa na serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania na kwamba wamefikia hatua za juu zaidi kubaini miamba yenye viashiria vya mafuta.
"Mwaka 2015 tukitumia ndege kubaini ukomo wa miamba hiyo na tuliweza kufanya tafiti mbalimbali katikati hapa...tulifanya Utafiti wa Kijiokemia mwaka 2021 na mwaka jana (2023) tulianza Utafiti Kwa njia ya mitetemo ya mfumo wa 2D, njia hii inasaidia kubaini kina Cha miamba pia kubaini mashapo yenye mkusanyiko wa Mafuta chini ya ardhi" amesema Maduhu.
Brayan Kamoga ambaye Meneja Msaidizi toka kampuni ya Utafiti ya Africa Geophisical Service (AGS) amesema wanashirikiana na serikali kutoa Elimu kwa umma kupitia viongozi wa vijiji ili kuhakikisha lengo la Mradi huo linafanikiwa.
0 Comments