Header Ads Widget

PROF. NDAKIDEMI "WANANCHI JITOKEZENI KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA MKAZI"

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


MBUNGE wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi  amewataka wananchi wa kata zote za Jimbo hilo kujiandikisha kwenye daftari la Mkazi ili kuweza kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuchagua viongozi bora na wanaowapenda.



Prof. Ndakidemi ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi waljitokeza kujiandikisha katika Kijiji cha Boro, Kata ya Kibosho Kirima. Mbunge Ndakidemi ni mzaliwa wa Kijijiji cha Boro.



“Napenda nichukue nafasi hii kuwaomba nyie mliomaliza zoezi hili leo mkawahimize wananchi wengine kwenye familia zetu, vitongoji, kijijini na kwenye Kata  kuhakikisha wanajiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura katika makazi yao wanakoishi hii itawawezesha kupiga kura Novemba 27 mwaka huu kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa mnaowapenda na watakao leta mafanikio katika maeneo yetu" Alisema Prof. Ndakidemi. 



Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI