Header Ads Widget

MHANDISI KUNDO APITA MTAANI KUHAMASISHA MAKUNDI MBALIMBALI KUJIANDIKISHA.


Matukio Daima Media-Simiyu.

MBUNGE wa Jimbo la Bariadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo  Mathew amejiandikisha kwenye Daftari la wakazi katika kitongoji cha Ng'hulo, kijiji cha Nkololo wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu huku akiwataka waliosalia kujitokeza kujiandikisha.

Akizungumza mara baada ya kujiandikisha mapema leo Oktoba 19, 2024, Mhandisi Kundo amewasisitiza wananchi kutumia vizuri muda uliobaki ili wasipoteze haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wa vitongoji na vijijiji.

Ameeleza kuwa  kujiandikisha ni hatua muhimu katika kuhakikisha ushiriki wao kwenye mchakato wa kidemokrasia wa kuchagua viongozi na kuchaguliwa.

Aidha, Mhandisi Kundo amewahamasisha makundi mbalimbali ikiwemo Wanawake, walemavu pamoja na Viongozi wa dini na kuwakumbusha kutumia vizuri siku zilizobaki kutimiza haki yao ya kikatiba.

"Tumieni haki yenu ya Kikatiba kujiandikisha ili kuchagua viongozi bora wa Serikali za Mitaa mwezi ujao...kila kura inahesabika na inaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye jamii, ikizingatiwa kuwa viongozi watakaochaguliwa watakuwa na jukumu la kusimamia maendeleo makubwa yanayoletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika mitaa,vitongoji na vijiji vyao." Amesisitiza Kundo.

Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wakazi la wapiga kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ulianza Oktoba 11, 2024 na utamalizika Oktoba 20, 2024.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI