Header Ads Widget

MAOMBI YA USHIRIKI TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARD YASOGEZWA MBELE

 


Na Fatma Ally Matukio DaimaApp, Dar

Chama Cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania (TAMWA) kwa Kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wamesema muda wa kuomba kushiriki tuzo za Samia Kalamu Awards umesogezwa mbele hadi Octoba 30, 2024.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam 

Mkurugenzi Mtendaji TAMWA Dkt Rose Reuben amesema kuwa awali tarehe ya mwisho kuwasilisha maombi hayo ilikua Octoba 26,2024 .


"Uamuzi huu wa kuongeza muda umechukuliwa ili kutoa nafasi Kwa wale waliokutana na changamoto za kiufundi ikiwemo kushindwa kupandisha kazi mitandaoni kutokana na matatizo ya Mtandao na changamoto nyingine"


Amesema kuwa, tuzo hizo zitatolewa Kwa wanahabari wa kitanzania zikiwa na lengo la kuhamasisha kukuza na kupanua wigo wa uandishi, utangazaji, na uchapishaji wa maudhui ya ndani kupitia vyombo vya habari vya asili na mtandaoni.


"ili kuchochea uandishi wa makala za kina zinazozingatia maendeleo, uwajibikaji, Mila na tamaduni pamoja kujenga chapati na taswira ya nchi yetu"


Ameongeza kuwa, kazi zilizowasilishwa na zinatakiwa kuwa za kipekee na ambazo hazijawahi kuwasilisha kuwania tuzo nyengine na zinazofuata taratibu za haki miliki ambapo waandishi wanatakiwa kuwasilisha kazi zao kupitia tovuti rasmi ya tuzo www.samiaawardds.tz.


Aidha, waandishi wa mikoa ambao hawajawasilisha maombi ya ushiriki watumie siku ambazo zimeongezwa kutuma kazi zao ili kuweza kushindania tuzo hiyo.


Mpaka sasa mikoa ambayo imewasilisha ni mikoa 23 ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Shinyanga, Mwanza, Mtwara, Simiyu, Geita, Iringa, Songwe, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora, Kagera, Mjini Magharibi, Ruvuma, Lindi, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, na Pwani.


Aidha, mchakato wa upigaji wa kura Kwa wananchi utaanza rasmi tarehe 8 Novemba 2024, hivyo, wanawahimiza wanahabari kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki katika kupiga kura Kwa wingi, kwani kura hizo zinachangua asilimia 60 ya alama za mshindi huku asilimia 40 zikiamukiwa na jopo la majaji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI