KUNDI la Tembo limevamia na kuharibu Miundo mbinu ya mashamba darasa ya umwagiliaji kwa njia ya matone ya mkulima Kiongozi kutoka jamii ya Wafugaji, Mathayo Olenyoke, yaliyopo katika Kijiji cha Orkirung'rung kata ya Endonyongijape, tarafa ya Naberera wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Kundi hilo la Tembo limefanya Uvamizi huo majira ya asubuhi, Oktoba 27 mwaka huu hali inayorudisha nyuma morali ya Wakulima Wafugaji wa Wilaya ya Simanjiro waliovutilka kuingia kwenye kilimo hicho kinacholenga pia kulinda, kuhifadhi na kutunza mazingira.
Hivi karibuni Olenyoke na familia yake walieleza mafanikio makubwa waliyopata kutokana na kilimo hasa cha Umwagiliaji, licha ya changamoto ya uhaba wa maji na ukame, hali iliyowafanya kuongeza mashamba mapya ya Kilimo cha maza umwagiliaji kwa mazao ya jamii ya Mikunde.
Mkulima Olenyoke hivi Karibuni alieleza kupata mafanikio makubwa kutokana na kilimo ikiwemo kujenga nyumba ya kisasa, kusomesha watoto hadi chuo kikuu, kuongeza mashamba na faida nyingine,
hamasa zaidi ikiwa ni baada ya elimu waliyopewa na taasisi ya kukuza na kuendeleza uchumi wa kimasoko, AMDT na Beula seeds kupitia mradi wa maono ya mabadiliko kwenye mazao ya udongo (VACS) WA unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa, USAID unaotekelezwa katika mikoa ya Manyara, Kilimanjaro, Arusha na Dodoma.
Pichani chini ni baadhi ya Miundombinu hiyo iliyoharibiwa na tembo hao:
0 Comments