Header Ads Widget

DC SIMALENGA MGUU KWA MGUU MTAANI KUHAMASISHA UANDIKISHAJI




MKUU wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Simon Simalenga ametembelea na kufanya mikutano na Wananchi katika kata za Bariadi, Nyakabindi, Nyangokolwa na Bunamhala kwa lengo la kuwahamasisha wananchi wajitokeze kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi ili waweze kushiriki Uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika Nov 27, 2024.

Simalenga amewataka wananchi hao kujitokeza kujiandikisha ili wawe na sifa ya kushiriki kupiga kura na kuchagua viongozi wa serikali za Mitaa wenye sifa.

Amewataka pia kuwa mabalozi kwa kuhamasisha wananchi  wengine wenye sifa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI