Header Ads Widget

DC MBOZI AHIMIZA WANANCHI KUJIANDIKISHA KUPATA VIONGOZI BORA.

 

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe Esther Mahawe, amewataka wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza kujiandikisha ili waweze kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vitongoji na vijiji utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Mahawe ametoa wito huo wakati wa kuhamasisha wananchi wa mji mdogo wa Mlowo kushiriki kujiandikisha ili waweze kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kuhakikisha wanapata viongozi wenye uelewa wa mahitaji yao. 

"Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni fursa muhimu kwa wananchi kuamua viongozi watakaowawakilisha katika ngazi za chini, hivyo ni muhimu kila mmoja kuchukua hatua ya kujiandikisha na kushiriki kwa wingikatika zoezi hilo" amesisitiza Dc Mahawe.


"Nimekuja leo kuzungumza nanyi kwa ajili ya kuwahamasisha kujiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura. 


Nimekuja mwenyewe inawezekana watu wanauchukulia poa uchaguzi huu, uchaguzi huu ndio unatupatia viongozi bora kutoka ngazi ya chini ili waweze kutuwakilisha vyema, hivyo mwananchi unaye nisikia usikubali kuchaguliwa viongozi jitokeze ili ukachague kiongozi unayemtaka", amesema Mhe. Mahawe ambaye alitumia guta kuwasili katika mji huo mdogo.


"Ninakusihi sana na tuwachague viongozi  bora sio bora viongozi, zoezi hili lilianza tarehe 11 mwezi huu mwisho tarehe 20 kajiandikishe katimize wajibu wako. Na bahati nzuri Wilaya ya Mbozi ina nusu ya wakazi wa Mkoa mzima tunategemewa sisi wana-Mbozi kwa idadi yetu tuhakikishe tuna ubeba mkoa na Taifa kwa ujumla", ameongeza kiongozi huyo wa wilaya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI