Header Ads Widget

DC LINDI AWATAKA VIJANA KUGOMBEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

 

Na Hadija Omary 

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bi.Victoria Mwanziva amewataka vijana Wilayani Humo  kushiriki kugombea Katika nafasi mbalimbali za uongozi Katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika November 27,2024

Mwanziva ametoa Rai hiyo Leo oktoba 27, 2024 alipokuwa anazungumza na MAAFISA usafirishaji wa pikipiki na bajaji (Bodaboda) Manispaa ya Lindi wakati wa tamasha la kuhamasisha wa wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopewa jina la safari ya uchaguzi 

Mwanziva Amesema vijana bado wananafasi kubwa ya kugombea na kuchaguliwa Katika Maeneo Yao na kwamba sifa za kugombea wanazo hivyo wajitokeze kigombea ili wawe miongoni mwa watoa maamuzi Katika Maeneo yao 

Hata hivyo aliwasisitiza kujitokeza kwa wingi siku ya November 27 kushiriki Katika kuchagua viongozi wanaowataka na wenye sifa za kuwaongoza Katika kipindi hicho


Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Lindi Juma Mnwele Amesema kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa November 27 mwaka huu tayari shughuli mbalimbali kinaendelea kufanyika ndani ya Manispaa hiyo

Amesema zoezi linaloendelea sasa ni uchukuaji wa fomu za wagombea ambalo limeanza rasmi oktoba 27 na litaitimishwa November 1 mwaka huu ambao alitoa wito kwa vijana na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za ugombea Katika wakati huo uliopangwa na Serikali 

Katibu wa chama cha waendesha boda Boda na Bajaji Manispaa ya Lindi Shabani kikotokeki amesema wapo tayari kushiriki kikamilifu Katika uchaguzi huo wa Serikali za mitaa ambapo Ameeleza kuwa tayari baadhi ya wanachama ama Bodaboda wameshachukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi hizo


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI