Header Ads Widget

BAGIDADI ATAFUTWA NA POLISI TANGA KWA KUUA MKE NA MFANYAKAZI KISHA KUWATOBOA MACHO..


 Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linamtafuta Alii Mohammed maarufu kwa jina Bagidadi, ( 60) Mkazi wa Barabara ya 4, Wilaya na Jiji la Tanga kwa tuhuma za kumuua Mke wake Saira Ali Mohammed, ( 50) na binti wa kazi anayejulikana kwa jina la Asha(20) kwa kuwanyonga na kamba aina ya katani shingoni kisha kuwatoboa macho.

Kamanda wa Polisi (M) Tanga ACP Almachius Mchunguzi  alisema kuwa tukio hili limetokea Septemba 30, 2024 majira ya saa 1:00 usiku na kwamba baada ya mtuhumiwa kufanya kitendo hicho alitorokea kusikojulikana.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linatoa wito kwa Wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mahali popote atakapooneka ili akamatwa na sheria iweze kuchukuwa mkondo wake.


Aidha, Jeshi la Polisi linawaasa Wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi yetu.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI