Header Ads Widget

AIDAN MLAWA -LEO NI SIKU YA MWISHO KUJIANDIKISHA AMBAO BADO ITUMIENI KUJIANDIKISHA

WAKATI Leo ni Siku ya Mwisho iliyopangwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi kujiandikisha mdau wa maendeleo Kilolo Aidan Mlawa amewahamasisha  wananchi ambao bado hawajajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kutumia siku hii ya mwisho kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa kikatiba.

Mlawa amesema kwa upande wake tayari amekwisha jiandikisha hivyo ni  umuhimu wa kila mmoja kujiandikisha kwani ni masaa machache yamebaki  kabla ya zoezi hilo kufungwa rasmi. 

Alisema kuwa ushiriki wa kila mwananchi katika uchaguzi ni haki na wajibu wa msingi wa kikatiba ambao unapaswa kuheshimiwa. Alifafanua kuwa bila kujiandikisha, wananchi wanapoteza fursa ya kuchagua viongozi wao na kushiriki katika maamuzi muhimu yanayohusu maendeleo ya wilaya na taifa kwa ujumla.

 "Ni vema Kila mmoja akatambua kuwa hii ni nafasi ya pekee ambayo kila mmoja anapaswa kuitumia ili kuhakikisha anakuwa sehemu ya mabadiliko ya kijamii na kisiasa yanayokuja," alisema Mlawa.

Mlawa alisema  kuwa serikali imetoa nafasi za kutosha kwa wananchi kujiandikisha, lakini bado kuna idadi ndogo ya watu ambao hawajafanikisha mchakato huo. rasia.


Hivyo aliwataka wale waliochelewa kutumia fursa hii ya mwisho na kuelekea vituoni mapema ili kuepuka msongamano wa dakika za mwisho. 

 Mlawa ambae ni mfanyabiashara anayeshanya shughuli zake jijini Dar es Salaam alisema ili wananchi waweze kupata viongozi Wazuri ni lazima kila mmoja akajiandikishe.

Mlawa alisema iwapo mtu hatajiandikisha  athari zake ni  kutoshiriki mchakato wa uchaguzi kunawaweka wananchi katika nafasi ya kupoteza sauti yao kwenye uongozi wa eneo lao. 

Kuwa ni muhimu tukumbuke kuwa uchaguzi siyo tu kuhusu kupiga kura bali pia ni kuhusu kujitokeza na kujiandikisha. 

Hata hivyo Mlawa amewashukuru wale ambao tayari wamejiandikisha kwa kujitokeza kwa wingi na kuwahamasisha wengine kufanya vivyo hivyo kabla ya kufungwa kwa zoezi hilo.

Alisema   kuwa ushirikiano wa wananchi ni wa maana sana katika kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa mafanikio na wa haki kwa pande zote.

Zoezi hili la kujiandikisha ni maandalizi muhimu kwa uchaguzi ujao, ambapo wananchi watakuwa na nafasi ya kuchagua viongozi wanaoamini watasimamia maendeleo ya Kilolo na kuboresha maisha yao kwa ujumla.

 Ikumbukwe kuwa vituo vyote vya kujiandikisha vimesalia wazi leo hadi muda wa jioni.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI