Khadija Mussa Haroun ni Afisa Afya wa Mkoa wa Iringa, ambae ameibuka mshindi wa tuzo ya heshima na hadhi kubwa, Tuzo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kama Afisa Bora wa Afya wa Mwaka.
Tuzo hii ni ushuhuda wa juhudi zake kubwa na za kipekee katika kuboresha sekta ya afya mkoani Iringa na kutambua mchango wake kwa ustawi wa jamii.
Katika mazingira ya changamoto zinazokabili sekta ya afya, mafanikio haya ya Khadija ni matokeo ya kujituma kwake, bidii, na ubunifu katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Iringa.
Kupitia tuzo hii ameonesha uongozi bora kwa kusimamia miradi muhimu ya afya, kuhakikisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi, na kushughulikia changamoto zinazowakabili wahudumu wa afya katika mkoa huo.
Kupitia uongozi wake, Mkoa wa Iringa umeendelea kuboresha viwango vya utoaji wa huduma za afya, kuhakikisha upatikanaji wa dawa, na kuimarisha miundombinu ya afya.
Pia, ameonyesha umahiri katika kutoa elimu ya afya kwa jamii, hasa katika maeneo ya vijijini ambako huduma za afya ni changamoto.
Hii imechangia kupunguza magonjwa ya milipuko na kuboresha hali ya afya ya wakazi wa mkoa wa Iringa.
Khadija Mussa Haroun ameweka alama isiyofutika katika historia ya afya ya mkoa huo kwa kuwa mstari wa mbele kupambana na magonjwa kama vile Malaria, Kipindupindu, na Ukimwi. Amehakikisha huduma za kinga zinawafikia wananchi wengi zaidi, huku akisisitiza umuhimu wa kinga kuliko tiba.
Tuzo hii ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inathibitisha kuwa uongozi bora, weledi, na kujituma vinaweza kuleta mabadiliko makubwa katika jamii.
Ushindi huu ni faraja siyo tu kwa Khadija, bali pia kwa wananchi wa Iringa, ambao wamefaidika moja kwa moja na jitihada zake za kuboresha afya zao.
Khadija amekuwa mfano wa kuigwa kwa maafisa wengine wa afya nchini. Ushindi wake unatoa motisha kwa watumishi wa umma wote kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kujituma kwa manufaa ya Watanzania.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuboresha sekta ya afya nchini, anapaswa pia kupongezwa kwa kutambua na kuthamini juhudi za watumishi kama Khadija.
Kwa niaba ya wananchi wa Iringa, tunatoa pongezi za dhati kwa Khadija Mussa Haroun kwa ushindi huu mkubwa.
Tunamtakia mafanikio zaidi katika kazi yake ya kutumikia jamii na kuendelea kuwa kiongozi wa mfano katika sekta ya afya.
Ushindi wake unatuonyesha kwamba, kwa bidii na kujituma, inawezekana kuboresha maisha ya wananchi na kuimarisha sekta ya afya nchini ndani ya mkoa wa Iringa na tuzo hii iwe chachu ya kusonga Mbele zaidi.
Kwa zaidi ya miezi miwili kuanzia mwaka 2022 Hadi 2024 matukio Daima media imekuwa ikiendesha Kampeni ya usafi wa Mazingira katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Iringa kwa kuibua maeneo machafu na kuripoti Kampeni ambayo ilichukiwa na baadhi ya viongozi wa wilaya na mkoa ila ndio iliyopelekea kuzaa matunda na Kuleta heshima hii kwa mkoa kupata tuzo ya Afya Afya Bora
0 Comments