Header Ads Widget

YASSIN -VIJANA MSIKUBALI KUTUMIKA NA WENYE NIA YA UBUNGE NA UDIWANI


Na Matukio Daima App 

Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Daudi Yassin amewataka Vijana kutokubali kutumika vibaya na watu wenye lengo la kutaka ubunge ama udiwani .

 Mbali ya kuwataka Vijana kujitambua Yassin amewaeleza  mambo muhimu 11 ya kuzingatia Vijana .

Akizungumza na Vijana jumuiya ya umoja wa Vijana wa Chama Cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa wakati akifungua mafunzo ya UVCCM wa mkoa wa Iringa katika chuo Cha Ihemi .

Yassin aliwataka Vijana hao 428 kutoka katika kata 107 ambao wanaendelea na mafunzo yanayofanyika kwenye chuo hicho cha UVCCM cha Ihemi kuzingatia Mafunzo pia Kufanyia kazi Mafunzo hayo muhimu Kuelekea  uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 mwaka huu.

Yassin alisema Jumuiya ya Vijana ndiyo Injini ya CCM na kwamba, lazima  watambue hilo.

Mambo aliyogusia kwenye mafunzo hayo ni kuhusu subira, kujitambua, uzalendo, kuwa wakweli wakati wote na kutokubali kutumika vibaya na wale wanaotaka.

Amewashauri vijana wawe jasiri  na sio legelege, waadilifu, waaminifu, wasiwasahau wazee na zaidi, wawe wakereketwa na kuhakikisha wanakipigania Chama cha Mapinduzi.

"Usiwe kijana mwenye kiburi na Mungu huwapa neema wabyenyekevu, tanguliza mbele maslahi ya CCM na sio maslahi yako. Kuweni na heshima," amesema Yassin.

UVCCM Mkoa wa Iringa chini ya Mwenyekiti wake Agrey Tonga na Katibu, Aisha Mpuya wameahidi kuisimamia jumuiya hiyo na kwamba itaendelea kuhakikisha inakipambania Chama cha Mapinduzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI