TAARIFA KWA UMMA
Kampuni ya Honora Tanzania Public Limited ("TIGO") inatambua taarifa za hivi karibuni kwenye vyombo vya habari kuhusu kesi inayoendelea ya ajira katika mahakama ya ajira ya London inayomuhusisha mfanyakazi wa zamani wa Millicom, kampuni mama ya Tigo hadi mwaka 2022.
Kampuni ya sasa mama ya Tigo haikuwa mmiliki wa Tigo wakati tukio hilo lilipotokea.
Ingawa hatuwezi kutoa maoni juu ya undani wa kesi hiyo, kwani hatuhusiki katika shauri hilo, tunapenda kuwahakikishia wateja wetu na wadau wetu kwamba kulinda taarifa zao binafsi kwa mujibu wa sheria na kanuni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado ni kipaumbele chetu cha juu zaidi.
MWANAHALISI WAMKOSEA WAZIRI LUKUVI WAOMBA RADHI ...
"Kumradhi Waziri Lukuvi"
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi, analengwa kuchafuliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Katika toleo lake la 26 Septemba mwaka huu, gazeti la MwanaHALISI liliripoti katika ukurasa wa mbele, kuwa Lukuvi anataka Rais Samia abakie madarakani hadi mwaka 2035, lakini mwenyewe amekana kutamka maneno hayo.
MwanaHALISI Online limeona video inayomuonyesha Lukuvi akizungumzia jambo hilo, lakini baada ya uchunguzi wake imeonyesha kuna kila dalili kuwa imehaririwa kwa nia mbaya.
Baada ya majadiliano ya kina na kiongozi huyo, tumekubaliana kwa kuchapisha maudhui hayo, tumemkosea na kwa sababu hiyo tunamuomba radhi.
Mhariri.
0 Comments