Header Ads Widget

RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN ATOA MAAGIZO KWA VIONGOZI WA WILAYA YA TUNDURU.

 


 NA AMON MTEGA, TUNDURU - RUVUMA 


RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi waliyopatiwadhamana ya kuwatumikia Wananchi katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma kukanusha mambo ya upotoswaji yanayofanywa na baadhi ya watu wasiyoyatakia mema maendeleo yanayofanywa na Serikali.


Agizo hilo amelitoa alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Tunduru Mkoani humo baada ya kupata taarifa kupitia mitandao ya kijamii iliyosema kumekuwepo na mgonjwa aliyebebwa machela kwa mfumo wa tenga katika kata ya Mchoteka Tarafa ya Nalasi wakati Serikali imetoa magari manne (4)ya kubebea wagonjwa katika Wilaya hiyo.



Rais ambaye yupo Mkoani humo kwenye ziara amesema kuwa Viongozi wamaeneo husika wanatakiwa kusimama na kukanusha mambo hayo ya uzushi kwa kuwa yanalenga kuichafua Serikali wakati Serikali imefanya mambo mengi ya maendeleo kwa Wananchi.


Amesema kuwa kama Viongozi wamaeneo husika wanaona uzushi kama huo lakini bado wananyamaza hawasemi ukweli basi kutakuwa na shida kwa Viongozi hao jambo ambalo amesema halileti picha nzuri kwenye maeneo yao ya kuwatumikia Wananchi.



Katika jambo hilo awali Waziri wa Tamisemi Mohamed Mchengerwa alimwambia Rais kuwa taarifa hiyo iliyorushwa na moja ya mitandao ya kijamii ni ya uzushi kwa kuwa watu hao wamekuwa wakichukua picha za zamani na kurusha kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha taharuki kwa Wananchi.


 Mchengerwa amesema Serikali ya awamu ya sita imetoa magari manne (4)ya kubebea wagonjwa na kumekuwepo na huduma ya M,mama hivyo haiwezi kufikia hatua ya kubeba mgonjwa kwenye machela wakati huduma zote zipo.



 Inadaiwa kuwa kata hiyo ya Mchoteka inaongonzwa na Diwani wa Chama Cha Upinzani na kuwa katika kipindi hiki tunachoelekea kwenye uchaguzi baadhi ya watu wasiyoyatakia mema maendeleo yanayofanywa na Serikali watakuwa wanapotosha jamii.


 Hata hivyo Mbunge wa Tunduru kasikazini  Hassan Kungu na Mbunge wa Tunduru kusini wamemshukuru Rais kwa kuwapatia fedha nyingi za ujenzi wa  miradi miradi mbalimbali.

      Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI