Na,Jusline Marco;Arusha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Mpango amesema mashirika ya dini yana mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa.
Akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Kilele cha Maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la New Lifu Outreach jijini Arusha,Dkt.Mpango amesema Serikali itaendelea kusimamia haki na Uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa Sheria na taratibu za Nchi.
Aidha amekemea baadhi ya madhehebu yanayotoa mafundisho potofu kwa waumini na kujilimbikizia fedha na Mali kutoka kwa wananchi wanyonge ambapo amewaomba viongozi wa dini kukemea vitendo vya kikatili vinavyoshamiri kila kukicha.
Waziri wa Mambo ya Nje Mhandisi Hamad Masauni amesema shirika hilo limekuwa ni mfano wa kuigwa kwa kutii Sheria na taratibu za nchi huku katibu wa jumuia ya maridhiano na Amani Tanzania Ask.Dkt.Israel Maasa akieleza kuwa umuhimu wa kuitunza Amani ya Nchi.
Kwa upande wake Mwasisi wa huduma hiyo Mwinjilisti Dkt.Egon Christian Falk amesema ili kuunga mkono jitihada za serikali,shirika hilo tangu kuanzishwa kwake limekuwa likifadhili zaidi ya wanafunzi 230 kwa kulipa ada za masomo huku wengine wakilipiwa ada pungufu kutokana na mazingira yao magumu ya maisha ambapo ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuikubali huduma hiyo kwa miaka yote 50.
Ameongeza kuwa kufanyika kwa maadhimisho hayo ya miaka 50 kumeenda sambamba kutimiza miaka 76 ya kuzaliwa kwake akiwa na watoto 3,uwepo wa chuo cha biblia,kanisa,shule 2 za msingi na shule 1 ya sekondari.
Awali Katibu Mkuu wa Kanisa hilo. Askofu Peter Rafael Mkilindi akisoma risala kwa mgeni rasmi amesema tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo mnamo mwaka 1974 ,chini ya Mwinjilisti Dkt.Egon Falk na mke wake waliweza kushirikiana na viongozi mbalimbali wa serikali na kutoa msaada mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule na utoaji wa madawati kwa ajili ya wanafunzi.
Pamoja na mafanikio hayo huduma hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zimegeuzwa kama fursa na kuiomba serikali kuangalia miundombinu ya barabara inayoelekea katika shule za huduma hiyo kwani watoto wamekuwa wakishindwa kupita hasa wakati wa mvua.
Hata hivyo sherehe ya miaka 50 ya New Life Outreach ilitanguliwa na huduma ya kutembelea hospitali ya seliani Ngaramtoni,gereza la kisongo Arusha,kituo cha watoto yatima na kufanya matendo ya huruma kwa kutoa chakula na mahitaji mbalimbali sambamba na kufanya usafi wa mazingira katika mitaa yote.
0 Comments