Na Pamela Mollel,Arusha
Serikali ya Awamu ya sita imewatoa hofu wawekeza wa tasisi Binafsi, Asasi za kiraia wanaotaka kuwekeza hapa Nchini kuwa hakitakuwa na usumbifu wa Aina yoyote kwa kuwekeza katika sekta mbali mbali watavyovutiwa Kuja kuwekeza, kwani kufanya hivyo itasaidia kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa Nchi na watu wake.
Hiyo yamebainishwa Waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa, Kitila Mkumbo wakati akifungua Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) iliyoanza rasmi leo Septemba 9, 2024 jijini Arusha ambapo amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Asasi za Kiraia nchini na kuwaondolea vikwazo vya Aina yoyote.
Prof. Mkumbo amesema, lengo kuu la serikali ni kuhakikisha ustawi wa watu wote unakuwa, na ili kufika huko ni vema zaidi kujifunza kupitia kwa watu, kuwa wabunifu na kutoa maoni katika kuhakikisha Dira ya Mendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 inaleta tija zaidi hususan katika uwekezaji kwenye elimu, miundombinu ikiwemo umeme wa uhakika.
‘’AZAKI zihakikishe zinaisemea jamii changamoto ambazo wanaziona na kutatuliwa ili kuisaidia serikali kuzishughulikia na si kuilalamikia kuwa haifanyi kazi ilihali hawajazibainisha ili zifanyiwe kazi na jamii iweze kupata mabadiliko’’. Amesema Mkumbo.
Amesema nchi zilizoendelea zimepiga hatua katika maendeleo kwa sababu ya umeme hivyo uwepo wa Bwawa la mwalimu Nyerere nchini Tanzania hadi kukamilika kwake utawezesha umeme kupatikana kwa wingi ikiwemo uchumi kukua kupitia viwanda vinavyozalisha bidhaa ndani ya nchi na kuuza bidhaa hizo nje ya nchi kwakushirikiana na sekta binafsi hususan za kilimo .
Naye rais wa Foundation For Civil Society (FCS), Dk Stigmata Tenga amesisita kuwa lazima mabadiliko ya watanzania yatokee kupitia AZAKI ambazo ndio husemea wananchi wenye changamoto mbalimbali katika sekta za afya ,elimu, miundombinu ya barabara ikiwemo utoaji wa fursa za fedha kupitia taasisi mbalimbali zinazowawezesha wananchi kujikwamua kimaisha kupitia mikopo yenye riba nafuu na kuongeza kuwa rasilimali watu ni muhimu kuzingatiwa katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Wakati huo huo, Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark Africa Elibariki Shammy amesema mkakati wa serikali ni kuhakikisha biashara za kidigitali zinakua zaidi kwa kushirikisha vijana kwa kasi kubwa kupitia biashara kwa kuwawekea mazingira rafiki yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zilizopo nchini.
Awali Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Isabelle Mignucci ameshukuru ushikiano kati ya serikali ya Tanzania na mashirika mbalimbali unaoleta tija katika maendeleo sanjari na kuhakikisha vijana wanapata fursa za maendeleo kupitia teknolojia na ubunifu unaoleta tija zaidi katika ukuaji wa uchumi.
0 Comments