Na, Matukio daima App,
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda ameeleza mpango wake wa kuufanya Mkoa wa Arusha, kuwa kimbilio la Vijana wenye kutaka kutimiza malengo yao ya kiuchumi na kijamii.
Rc, Makonda ameyazungumza hayo wakati akielezea namna alivyojipanga kutekeleza maelekezo ya Serikali ya awamu ya sita ya chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kwasihii wananchi wa mkoa huo kuendelea kudumisha amani.
"Yote haya hayawezi kutimia bila kuwa na amani, hatuwezi kufanikiwa bila kuwa na amani na wewe mwananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla ndiyo mtunzaji wa amani, hakuna biashara itakayofanyika bila amani, viwanda haviwezekani kwenye vita, hakuna Mkulima atakayetoka na jembe kwenye vita na hakuna mtalii atakayekuja kwenye vita."amesema Mhe. Makonda.
Aidha, Makonda amesema kuwa mkoa wa Arusha inaenda kuwa kituo muhimu cha Utalii wa matibabu,Utalii wa mikutano na michezo pamoja na ufufuaji na uanzishaji mkubwa wa viwanda vya kuongeza thamani kwa mazao ya kilimo hasa cha mbogamboga na matunda, huku akiwaalika Vijana kwenda kuzitumia fursa hizo ili kuondokana na utegemezi.
0 Comments