Header Ads Widget

PUNDA,MBWA WAONDOLEWA KATIKA ORODHA YA WANYAMA WANAOLIWA

 


Na Thobias Mwanakatwe,DODOMA


WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imefanya maboresho ya kanuni kwa kumuondoa mnyama punda na mbwa katika orodha ya wanyama wanaotakiwa kuchinjwa na kufanywa kitoweo lengo ni kudhibiti biashara haramu ya nyama ya punda hapa nchini.


Naibu Mkurugenzi wa Haki za Wanyama na Ustawi wa Wanyama,Dk.Annette Kitambi,  alisema hayo juzi wakati wakati wa warsha ya wadau ya uwasirishaji wa tathimini ya ustawi wa wanyama inayofanyia mjini hapa.



Alisema marekebisho ya kanuni hiyo yatasaidia kumlinda mnyama Punda ambaye katika baadhi ya mikoa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na kasi kubwa ya kuchinja mnyama huyo kufanywa kitoweo jambo ambalo linahatarisha kutoweka kwa punda nchini.


Dk.Kitambi alisema hatua nyingine zinazochukuliwa na serikali ni kufanya marekebisho kwenye mitaala ya mafunzo ili baadhi ya wanyama akiwamo punda waweze kutajwa vizuri na hivyo wasiweze kupotea nchini.



"Katika kuhakikisha punda wanakuwa wengi nchini, tumeona kuna umuhimu wa kufanya utafiti wa uzalianaji wa punda maana inawezekana tatizo la punda kutozaliana kwa wingi linazababishwa na matunzo duni anayopewa," alisema.


Dk.Kitambi alisema pia serikali imekuwa ikitoa elimu ya ustawi wa mnyama punda kwenye minada,TV na redio,uteuzi wa wakaguzi wa masuala ya ustawi wa wanyama katika mamlaka za serikali za nitaa na uteuzi wa bodi ya kumshauri waziri masuala ya ustawi wa wanyama nchini.



"Mara nyingi punda anabebeshwa mizigo zaidi kile anachostahili kubeba wengi wanasema wewe mbebeshe mpaka atakapoanguka hapo ndipo mzigo unamtosha," alisema.


Naye Daktari wa Mifugo kutoka sekta binafsi, Dk.Bedan Masuruli, akiwasilisha ropiti ya tathimini ya hali mnyama punda, alisema licha ya katazo la serikali lililotolewa 2021 lakini bado biashara ya punda na nyama yake inaendelea kufanyika hapa nchini.



"Uzuiaji uchinjaji punda ni kama ulihusu tu kiwanda cha kusindika nyama ya punda cga Fang Hua kilichokuwa mkoani Shinyanga lakini licha ya katazo uchinjaji bado unaendelea na wizara inatoa vibari vya usafirishaji punda kama kawaida," alisema.


Dk.Masuruli alisema hivi sasa punda wengi kutoka mikoa mbalimbali wanasafirishwa kupelekwa Mkoa wa Geita lakini bado haijafahamika wakipelekwa huko baada ya hapo wanapelekwa wapi.


Alisema hata biashara ya ngozi ya punda bado inafanyika kwa kasi sana na pia punda wanasafirishwa kutoka Tanzania kupelekwa nchi jirani ya Kenya.


Alisema kuna haja kwa serikali ya Tanzania ishirikiane na serikali ya Kenya kudhibiti biashara ya punda kwani hivi sasa soko kubwa la punda linaonekana lipo Kenya.


Naye Mkurugenzi wa Shirika la Inades Formation Tanzania (IFTz),Mbarwa Kivuyo,alisema shirika hilo kwa kushirikiana na Brooker East Africa wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha haki na ustawi wa mnyama punda analindwa na kustawi.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI