"Kumbe mwamba huwa ananifuatilia. Si walisema nipuuzwe? Niliomba hoja zangu zijibiwe, na baadhi ya viongozi wandamizi wa Chadema' wamesisistiza hoja zangu zijibiwe. Freeman (Mbwe) wacha nikukumbushe kirafiki, 'tatizo la kisiasa linahitaji suluhu ya kisisa'. Nitaacha hakimu aamue"-Msigwa.
Maneno ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyassa, Mchungaji Peter Msigwa kupitia ukurasa wake wa X (Twitter), baada ya mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe kumtaka aomba radhi na kulipa fidia ya Shilingi bilioni 5 kutokana na madai ya kumkashifu na kuharibu chapa yake hadharani kwa maneno ya 'kashfa' baada ya yeye Msigwa kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
0 Comments