Na Editha Karlo,Kigoma
MKUU wa kikosi cha usalama barabarani (RTO)Mkoa wa Kigoma Timotheo Leonard Chikoti amezindua mashindo ya mpira wa miguu kwa timu za madereva bodaboda wa Mkoa wa Kigoma ambayo yanaendeshwa na kituo cha Radio cha Main FM.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mashindano hayo aliupongeza uongozi wa Main FM kwa kwa kuwakutanisha vijana wa boda boda kupitia mchezo wa mpira wa miguu na kuwataka wadau wengine wa michezo kuiga mfano huo.
Chikoti alisema bodaboda ni maofisa usafirishaji nanu kiungo muhimu kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi hivo kuwataka vijana kuendelea kuwa walinzi wa amani ya nchi kwa kuhakikisha hawashiriki katika matendo maovu na kufichua wahalifu.
“Nyie ni watu muhimu katika nyanja hii ya usafirishaji,serikali na wadau mbalimbali wanaendelea kushirikiana na nyie kwenye mambo ya kijamii kama hivi mashindo ya mpira ambayo Main FM watayaendesha hivi karibuni”alisema
Naye Mkurugenzi wa Radio ya Main FM Pasco William alisema wanatambua mchango wa bodaboda katika jamii kwa kutoa huduma ya usafiri kwa haraka na wakati hivo tumeamua tushirikiane nao kupitia michezo.
Alisema Mashindano hayo yataanza tarehe 28 mwezi wa kumi yatashirikisha timu tisa toka Manispaa ya Kigoma ujiji na Halmashauri ya Kigoma ambapo mshindi wa kwanza atapewa zawadi ya shilingi milioni moja na mshindi wa pili shilingi laki tano.
Naye Mwenyekiti wa umoja wa bodaboda Mkoa wa Kigoma Samwel Lamek Joseph aliushukuru uongozi wa Radio ya Main FM kwa kutambua mchango wa madereva bodaboda na kuamua kuanzisha ligi hiyo ambayo itawakutanisha na kutoa burudani kwa mashabiki pamoja na kujenga afya zao.
0 Comments